Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma yahimiza ukweli, uwajibikaji

Katibu Idara ya Ukaguzi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha, akifungua kikao kazi kwa niaba ya Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi. Kikao hicho kimehusisha wadau mbalimbali kutoka wizara, idara na taasisi zinazojihusisha na utoaji wa elimu kwa umma, kwa lengo la kuweka mikakati ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maadili ya viongozi wa umma. Picha na Hamida Shariff.

Muktasari:

  • Mambo saba yanayopaswa kuelimishwa kwenye jamii na viongozi wa umma ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka kwa masilahi binafsi, kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji katika maamuzi, rushwa, vitendo vya upendeleo na maadili ya kazi na mgongano wa masilahi.

Morogoro. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewataka wadau wanaotoa elimu kutoka taasisi za Serikali na mashirika ya umma kuzingatia weledi, ukweli na uwajibikaji katika utoaji wa habari ili kuhakikisha taarifa zinazotolewa zinajenga na si kubomoa jamii.

Akifungua kikao kazi cha wadau wa utoaji elimu kwa umma kutoka wizara, idara, taasisi za Serikali na mashirika ya umma, Katibu Idara ya Ukaguzi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha amesema, licha ya jitihada mbalimbali zinazofanyika, bado sekretarieti hiyo inahitaji kushirikiana na wataalamu wengine ili kufikia lengo na kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa maadili.

“Waswahili wanasema kidole kimoja hakivunji chawa ndio maana tumewaiteni hapa tubadilishane mawazo kuhusu njia na mbinu bora za utoaji elimu kwa umma zitakazosaidia kutimiza malengo yetu kwa pamoja na lengo hili likitimia litapunguza changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa letu," amesema Kipacha.

Amesema baadhi ya changamoto wanazotakiwa kukabiliana nazo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi na watumishi ni matumizi mabaya ya madaraka kwa maslahi binafsi, kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji katika maamuzi.

Ametaja eneo lingine ni rushwa, vitendo vya upendeleo, kutokutoa taarifa sahihi kwa umma, ukiukwaji wa misingi ya uongozi bora, maadili ya kazi na mgongano wa maslahi.

“Sekretarieti ya maadili, tunaona ni muhimu kushirikiana na taasisi mbalimbali za umma hususani watumishi wanaofanya kazi ya kutoa elimu kwa umma kukabiliana na changamoto hizi,” amesema.

Naye Mshiriki wa kikao hicho, Ofisa Habari Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Prudence Constantine amesema kazi ya Bodi hiyo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma na wanakuwa endelevu katika taaluma yao.

Prudence amesema tangu bodi hiyo ianze kazi waandishi wa habari zaidi ya 4,600 wamesajiliwa, huku 3,800 kati yao wakiwa  wameshapata ithibati na wanafahamika kwamba ni waandishi wa habari kisheria.