Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sendiga: Tuungane kupinga ukatili wa kijinsia

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga

Muktasari:

  • Matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Manyara, yamefikia 8,360 hadi Desemba mwaka jana 2023

Babati. Mkuu wa Mkoa wa Manyara , Queen Sendiga ameitaka jamii kubadili ili kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Sendiga ametoa wito leo Machi 23, 2024 na Mkuu wa mkoa huo, Queen Sendiga mjini Babati katika kikao cha kujadili hali ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye mkoani humo.

Takwimu za matukio ya ukatili mkoani humo zinaonyesha kuwa bado yanaendelea ambapo hadi Desemba mwaka 2023 yalifikia 8,360.

Hata hivyo, wilaya ya Hanang' bado inaongoza kwenye mkoa huo ambapo kwa mwaka jana pekee yamefanyika matukio ya ukatili 2,885.

Amesisitiza kuwa ili vitendo hivyo vikomeshwe, kila mtu anapaswa kuwa mstari wa mbele kuvikemea  kwa kutoa taarifa ngazi husika anapoona viashiria vya ukatili.

"Jamii inapaswa kubadilika kwa kuachana na ukatili wa kijinsia na pia matukio yasifumbiwe macho yanatakiwa kutolewa taarifa kwenye ngazi husika," amesema Sendiga.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameliomba Jeshi la Polisi kutowaachilia watuhumiwa wanapofikishwa vituoni.

Mkazi wa mji mdogo wa Katesh, Solomon Awet amesema watuhumiwa wanapokamatwa  na kufikishwa Polisi sheria ichukue mkondo wake.

Mkazi mwingine wa mji mdogo wa Katesh, Magdalena Asechek amesema matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yaliyokithiri wilayani Hanang' ni ukeketaji, na ndoa za utotoni.

"Watuhumiwa wanapokutwa na hatia ya kufanya ukatili wanatakiwa watumikie kifungo ili iwe onyo kwa wengine wanaoshiriki kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia," amesema Asechek.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, George Katabazi amesema watuhumiwa wote wa matukio hayo wakikamatwa huwa wanafikishwa mahakamani.

Amesema Polisi hawana huruma na watuhumiwa wote wa matukio ya ukatili wa kijinsia, hivyo wanachukuliwa hatua kwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.