Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali: Hakuna hitaji marekebisho sheria ya TIC

Serikali: Hakuna hitaji marekebisho sheria ya TIC

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema hadi sasa hakuna hitaji la kufanya marekebisho sheria ya Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema hadi sasa hakuna hitaji la kufanya marekebisho sheria ya Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Hayo yameelezwa leo Jumanne Februari 9, 2021 na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Patrobas Katambi wakati akijibu swali la mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi bungeni mjini Dodoma.

Chumi amesema vibali vya kazi vinavyotolewa nchini ni vya muda mfupi wakati baadhi ya uwekezaji ni wa muda mrefu, “serikali iko tayari kuongeza muda wa vibali kuvutia wawekezaji?”

Mbunge huyo pia alihoji Serikali kama haioni haja ya kufanyia marekebisho sheria ya  TIC.

Katika majibu yake Katambi amesema sheria inatoa nafasi ya mwekezaji kutoa ajira za watu watano kutoka nje ya nchi na kwamba anapewa fursa hiyo bila masharti yote ikiwa ni sehemu ya motisha.