Serikali kuchukua hatua wanaokiuka haki za wafanyakazi wa ndani

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Ajira na Kazi), Patrobas Katambi
Muktasari:
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Ajira na Kazi), Patrobas Katambi ametoa onyo kwa waajiri wanaovunja haki za wafanyakazi wa ndani, wanaonyima mikataba wafanyakazi na wale wanaoajiri watoto wadogo akisema Serikali inaendelea kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayoifikia ofisi yake.
Dodoma. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Ajira na Kazi), Patrobas Katambi ametoa onyo kwa waajiri wanaovunja haki za wafanyakazi wa ndani, wanaonyima mikataba wafanyakazi na wale wanaoajiri watoto wadogo akisema Serikali inaendelea kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayoifikia ofisi yake.
Katambi ameyasema hayo leo Januari 08 2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na vijana na kuahidi utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia aliyoyatoa Zanzibar kuhusu Haki na Wajibu wa Vijana kwenye ujenzi wa Taifa huku akigusia haki za Wafanyakazi wa ndani.
Ambapo amesisisitiza kuwa 'Wafanyakazi wa ndani Domestic Workers ( VIJANA -Wakike na Wakiume) aghalabu Wanawake (Jeshi la Mama yetu Amiri Jeshi SHH), pamoja na kuwa Dunia ya Leo ni ya Utandawazi lakini ndio wamegeuka Wazazi Walezi na Walimu Wakuu wa Tabia na Maaadili ya Watoto wengi kizazi kipya Wanapitia mengi mazito: Vipigo, Kutengwa, kudhalilishwa na Kubakwa, Manyanyaso aina zote na ngono, Dhuruma, Mimba Chini ya umri, nk hata ulemavu na vifo, Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (2004) RE 2019 inataka mtumishi awe na miaka 18 na 14 kwa masharti ilikutovunja kifungu Cha 5 (1)&(2) na 20(2) Sheria tajwa. Ni bahati mbaya tafiti zangu zinaonesha Wafanyakazi hawa wenye umri wa miaka 18 hawapendwi na Mama Wenyenyukba kwa hofu ya kupora Waume zao au hawana uwezo wa kuwanyanyasa na HouseBoy wa miaka 18 Waume huhofia wake zao au kutoweza kuwanyanyasa au kudhurumu kwani tayari wao na umri tambuzi. Wanachukua Watoto wadogo na kuwanyima Haki zao na best interest/ustawi kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto 2009'.
'Ni Wakati Sasa wa kuisikiliza jamii kuweka nguvu na kuzingatia Sheria yetu ya Ajira na Mahusiano Kazini (2004), RE: 2019 na International Domestic Workers Convention No. 189 ambayo Tanzania tumesaini na kuridhia (Signed &Ratified)'
Katambi amesema Ofisi yake iko wazi kwa yoyote anaemuona Housegirl au Houseboy alie chini ya umri kutoa taarifa Ofisini kwake na yoyote ambaye haki yake ya kazini au Ajira aliyonayo haipati sababu Serikali inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan imejizatiti zaidi kwenye utoaji haki na usimamiaji wa Wananchi kwenye Sheria.