Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali, wadau kuimarisha vita dhidi ya ukatili wa watoto

Watoto wa Shule mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Familia wilayani Karatu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mazingira Bora, Juni 30, 2026. Picha na Filbert Rweyemamu

Muktasari:

  • Katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Familia wilayani Karatu, Serikali na mashirika ya kiraia wamezitaka familia na jamii kuongeza ulinzi kwa watoto.

Arusha. Serikali, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wamezitaka familia na jamii kuongeza ulinzi kwa watoto huku wakionya kuwa kuendelea kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kunahatarisha ustawi wa kizazi cha sasa na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Familia yaliyofanyika leo Jumanne, Juni 30, 2026 kwenye uwanja wa Mazingira Bora ambapo watoto walidai haki yao ya kupata elimu bora, malezi salama pamoja na kupinga ukatili na unyanyasaji unaoendelea kujitokeza katika jamii mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dk Lameck Karanga aliwataka wananchi kuongeza ulinzi kwa watoto akisema watoto wa leo ndio msingi wa taifa la kesho, akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazoendelea kuonyesha katika kusimamia ustawi wa watoto nchini na kuweka mbele ajenda ya haki za mtoto.

Amewashukuru pia wadau waliofanikisha maadhimisho hayo wakiwemo pamoja na mashirika mengine ya kijamii kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda haki za watoto.

Watoto wa Shule mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Familia wilayani Karatu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mazingira Bora, Juni 30, 2026. Picha na Filbert Rweyemamu

“Tusione mtoto akiwa katika mazingira mabaya halafu tukasema sio wa kwangu. Mtoto ni mtoto na kila mmoja ana wajibu wa kumlinda,” amesema Dk Karanga.

Mkuu huyo wa wilaya amewaasa wazazi kufuatilia kwa karibu maisha ya watoto wao, kuwalinda dhidi ya mazingira hatarishi, matumizi ya pombe, ukatili wa kijinsia na kuhakikisha wanapata haki zote za msingi ikiwemo elimu, malezi bora, chakula, makazi salama pamoja na uangalizi wa karibu kutoka kwa wazazi na walezi.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa wilaya hiyo, Raymond Mushi amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya mtoto imeendelea kutekeleza mikakati ya kuboresha ustawi wa watoto ambapo familia 14 zimepatiwa mafunzo ya malezi chanya.

Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wazazi uwezo wa kuwalea watoto katika mazingira bora, huku familia nyingine 28 zikiwezeshwa kiuchumi kwa kupewa vifaa vya biashara ili kuongeza kipato na kusaidia kugharamia mahitaji muhimu ya watoto.

Amesema zaidi ya Sh40 milioni zimetolewa kupitia ushirikiano kati ya Serikali na wadau kwa ajili ya kutekeleza programu mbalimbali za maendeleo ya mtoto zikiwemo lishe, elimu, malezi bora pamoja na huduma za kijamii kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Juhudi hizo zimehusisha utoaji wa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya mtoto katika shule za msingi na sekondari, huku mifumo ya ushiriki wa watoto ikiimarishwa kupitia kuundwa kwa klabu za watoto, madawati maalumu ya watoto pamoja na mabaraza ya watoto yanayosaidia kutoa taarifa kuhusu changamoto zinazowakabili watoto katika jamii.

Watoto wa Shule mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Familia wilayani Karatu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mazingira Bora, Juni 30, 2026. Picha na Filbert Rweyemamu

“Halmashauri yetu imeendelea kusimamia watoto waliopoteza malezi ya familia, wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na wa mitaani kwa kuwapatia malezi mbadala na kuwaunganisha tena na familia zao pale inapowezekana,” amesema Mushi.

Takwimu zilizowasilishwa zinaonyesha kuwa jumla ya matukio 21 ya ukatili dhidi ya watoto yameripotiwa katika kipindi cha tathmini, ambapo kesi mbili zilihusu ubakaji, kesi nne ulawiti, kesi mbili kuwapa mimba wanafunzi na kesi 12 zilihusu mashambulizi ya aibu.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo, Ofisa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Fidelis Joseph amesema taasisi hiyo imeendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mtoto kwa kuanzia ngazi ya jamii ambako changamoto nyingi huanzia.

Amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuunda mabaraza 43 ya watoto pamoja na madawati 43 kwa kushirikiana na idara za ustawi wa jamii ili kuwajengea watoto mazingira salama ya kushiriki katika masuala yanayowahusu pamoja na kutoa taarifa pale wanapokutana na changamoto.