Serikali yaanza utekelezaji agizo la Chongolo
Naibu Waziri Tamisemi, David Silinde.
Muktasari:
- Agizo la ulinganifu wa walimu katika maeneo ya mijini na vijijini limeanza kutekelezwa Morogoro, walimu 545 wahamishiwa vijijini.
Dar es Salaam. Serikali imeanza utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo la kuhakikisha kuna uwiano wa kutosha kati ya walimu walio vijijini na mijini.
Akizungumza leo wakati maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa CCM, Naibu Waziri Tamisemi, David Silinde amesema agizo hilo limeanza kutekelezwa ndani ya siku saba tangu kutokewa kwake.
Amesema utekelezaji wa agizo hilo umeanzia katika Mkoa wa Morogoro ambapo walimu 545 waliokuwa mijini wameshapewa barua za kuhamishiwa vijijini.
“Tumeshatoa barua kwa walimu 545 kutoka Mkoa wa Morogoro kwenda maeneo ya vijijini na tumeshatoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo Sh607 milioni kwa ajili ya kuwasambaza.
“Hii ni awamu ya kwanza ila kazi ya kuwasambaza walimu inaendelea katika kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa walimu katika maeneo yote,”amesema Silinde.