Serikali yakanusha kuwarudisha kazini waliobainika kutumia vyeti feki
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora, Mohamed Mchengerwa
Muktasari:
- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali haijawarudisha kazini watumishi 5,335 waliobainika kutumia vyeti feki vya kidato cha nne, sita na ualimu.
Arusha. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali haijawarudisha kazini watumishi 5,335 waliobainika kutumia vyeti feki vya kidato cha nne, sita na ualimu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha leo Novemba 5, 2021 amesema Wizara haijatoa kibali cha kuwarudisha kazini watumishi hao waliobainika kutumia vyeti feki na kutoa taarifa za uongo za ajira.
Amesema msamaha ulitolewa na Serikali wa kuwalipa mafao au kuwarejesha kazini ni kwa watumishi pekee waliondolewa kimakosa.
Mchengerwa ameongeza kuwa wamefanikiwa kuwaondoa katika orodha ya mishahara watumishi hewa 19,708 na kuiwezesha Serikali kuokoa jumla ya Sh19.84 bilioni.