Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaokoa watu 182 usafirishaji haramu wa binadamu

Mjumbe wa Kitaifa wa Sekretarieti ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Inspekta Selestine Makoba (wa kwanza kushoto), akizungumzia namna Serikali ilivyowarejesha watu 182 waliokuwa wamesafirishwa kiharamu nchini. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuwaokoa watu 182 waliokuwa wamesafirishwa kiharamu ndani na nje ya nchi ndani ya mwaka mmoja huku baadhi yao wakiokolewa kutoka Asia.

Moshi. Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuwaokoa watu 182 waliokuwa wamesafirishwa kiharamu ndani na nje ya nchi ndani ya mwaka mmoja huku baadhi yao wakiokolewa kutoka Asia.

Miongoni mwa manusura hao ambao ni wanawake na watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 wamekuwa wakisafirishwa kwa utaratibu usio halali kwa ajili ya kwenda kutumikishwa kazi ngumu za nyumbani na kingono bila wao kujua.

Akizungumza katika Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Courage Worldwide mkoani Kilimanjaro, Mjumbe wa Kitaifa wa Sekretarieti ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Inspekta Selestine Makoba amesema Serikali imefanikiwa kuwarejesha manusura hao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Makoba amesema Serikali pia kwa kushirikiana na wadau wengine waliweza kuokoa walemavu tisa kati ya manusura 182 waliosafirishwa kwa njia haramu na kupelekwa nchini Kenya ambapo baadaye walifanikiwa kuwarejesha hapa nchini.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali imeweza kuokoa manusura 182 wengi wao ni wanawake na watoto wakiwa ni wa hapa ndani ya nchi na wengine tuliwaokoa kutoka Asia na mashariki ya mbali ambapo watoto wengi walikuwa chini ya umri wa miaka 18 ," amesema Inspekta Makoba

"Serikali tutaendelea kuzuia kwa nguvu zote magendo ya kibinadamu na usafirishaji haramu wa binadamu na Serikali imedhamiria kuhakikisha usafirishaji huu haramu unatokomea kabisa hapa nchini,"

Amesema katika kukabiliana na wimbi hilo Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali ambapo mpaka sasa imetoa mafunzo kwa watu 573 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mwenyekiti wa mtandao wa Kitaifa wa kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu nchini, Edwin Mgabira amesema ipo haja ya Serikali kufanya mabadiliko katika baadhi ya vifungu vya sheria ili kuwabana na kutokutoa mwanya kwa wale wanaofanya au wanaotaka kufanya biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu.

"Zipo baadhi ya changamoto kwenye vifungu vyetu vya sheria, tunaona sheria zinatoa mwanya kuwa mtu aliyefanya kosa la kusafirisha binadamu kulipa faini ya Sh5 milioni au Sh15 milioni ili akwepe kifungo jela, hii ni kikwazo kwetu sisi wadau ambao tunapambana na biashara hii,"

"Kwa mujibu wa ripoti za Kimataifa hawa watu wanaosafirisha binadamu wanatengeneza zaidi ya Sh150 bilioni dola za kimarekani kwa mwaka, halafu anafanya kosa anaambiwa alipe faini ya Sh5 milioni au Sh15 milioni hii haiingii akilini, hivyo ipo haya ya Serikali kuangalia hizi sheria upya,"

Mkurugenzi wa Shirika la Courage World wide, Jane Williamson alisema tatizo la usafirishaji wa binadamu ni kubwa na katika wanawake 10 wanaosafirishwa kati yao unakuta kuna watoto wadogo hali ambayo amesema jamii inayowajibu mkubwa wa kuwa waangalifu kwa watoto wao ili kuepusha hali hiyo.

Kwa upande wake Askofu mstaafu wa Kanisa la TAG Mkoa wa Kilimanjaro na Mchungaji kiongozi wa kanisa la KICC, Glorious Shoo amesema changamoto ya usafirishaji wa binadamu kwenye jamii ni kubwa kwa kuwa wapo baadhi ya wanajamii ambao wamekuwa wakisafirisha wasichana wa kazi kwenda mikoa mingine na mishahara yao wanakuwa wakiipokea wao.