Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yasema haijasitisha usafirishaji mazao ya chakula nje

Muktasari:

Wizara ya Kilimo imesema kuwa haijasitisha utoaji wa vibali vya kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi.

Dar es Salaam. Serikali imesema kuwa haijasitisha utoaji wa vibali vya kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Kilimo imesema kuwa wizara hiyo imeendelea kutoa vibali vya kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi kupitia mfumo wa utoaji vibali wa kielektroniki.

“Katika kipindi cha kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 7, 2022, Wizara imetoa vibali vya mahindi, maharage, unga na mchele kwenda nje ya nchi vyenye jumla ya tani 37,450” imesema taarifa hiyo.

Wizara hiyo imewataka wafanyabiashara wa mazao ya chakula kwenda nje ya nchi (Export) au kuingiza ndani ya nchi (Import) kufuata taratibu zilizopo.

“Kampuni inapaswa kuwa imesajiliwa na Brela au kwa kuzingatia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuwa na Leseni halali ya kufanya biashara ya Mazao ya Chakula, Nyaraka za kulipa kodi pamoja na Risiti ya EFD ya malipo kutoka Halmashauri husika ili kuepusha usumbufu usio wa lazima”

Wizara inawakumbusha wafanyabiashara wa mazao ya chakula kuwa, ili kuepuka usumbufu usio wa lazima, wanatakiwa kuwa na kibali cha kusafirisha mazao nje ya nchi (Export Permit) au

kuingiza ndani ya nchi (Import Permit) kabla ya kufikisha mzigo Mpakani, Bandarini, au Kiwanja cha ndege” imesema taarifa hiyo.