Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatakiwa kurasimisha ardhi kumaliza migogoro

Baadhi ya wananchi  jijini Arusha  wakipata  elimu kutoka kwa wataalamu wa  kituo cha LHRC katika soko la Mbauda jijini Arusha

Muktasari:

Wadau wa sheria mkoani Arusha waiomba serikali kuendelea na zoezi la urasimishaji ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi.

Arusha. Wadau wa sheria mkoani Arusha, wamesema kuwa kesi za migogoro ya ardhi bado ni changamoto kubwa kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini kutokana na elimu duni ya wananchi kuhusu sekta hiyo.

 Aidha kutokana na changamoto hiyo, wameiomba Serikali kuendeleza urasimishaji ardhi ili wananchi wawe na maeneo yanayotambulika kisheria na kuondoka na migogoro hiyo ambayo imekuwa sugu katika mikoa hiyo.
Akizungumza leo Oktoba 24  jijini Arusha wakati akitoa msaada wa kisheria katika wiki ya Azaki, kwenye maeneo ya soko la Mbauda na Kilombero, Mratibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Hamisi Mayombo amesema kuwa, katika utoaji wa msaada wa kisheria kwa Kanda ya Kaskazini wamebaini kesi nyingi ni za migogoro ya ardhi na masuala ya ajira.
"Kutokana na utitiri wa kesi hizi za ardhi sisi wadau wa sheria tunaomba serikali iendelee na zoezi la urasimishaji maeneo kwani maeneo yakipimwa itasaidia kupunguza migogoro hii," amesema.
Aidha ameshauri kuwe na mabaraza ya ardhi zaidi ya moja kwa wilaya zenye watu wengi kama Arusha na kwingine kuwepo moja kwa kila wilaya ili kuharakisha mashauri ya kesi hizo.
Amesema kuwa, kwa sasa kuna  changamoto kubwa  katika kusuluhisha kesi hizo na zinalundikana kutokana na kuwa na baraza moja kwa wilaya ya Arusha ambalo linahudumia wilaya ya Longido, Monduli na kwingine.

"Naishauri Serikali kuitazama upya sheria na sera za ardhi na urasimishaji ardhi na itungwe kulingana na matatizo yaliyopo ili kuweza kutatua changamoto hizo na wananchi kuweza kupata haki zao za msingi," amesema Wakili Mayombo.
Mayombo amesema kwa upande wa ajira kesi nyingi zimetokana na janga la Uviko-19 ambapo waajiri wengi walishindwa kulipa watumishi wao mishahara na kukatiza mikataba bila kufuata sheria.
"Wananchi wengi hawazifahamu haki zao ndo maana tumeamua kuitumia wiki hii kuhakikisha tunatoa elimu ya kutosha ili wananchi waweze kupata elimu ya kutosha na kujua  taratibu za kufuata "amesema Wakili Mayombo.
Kwa upande wake Ofisa Sheria kutoka LHRC, Amani Mkwama amesema katika msaada wa kisheria wanaoutoa wamebaini uwepo wa watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo wanaohitaji msaada wa mawakili mahakamani na baadhi kuandikishwa nyaraka za kisheria.
"Kila mmoja tunamsaidia kulingana na hitaji lake, hivyo tunawaomba wananchi kujitokeza kuja kupata msada huu bire hats wenye migogoro ya kifamiliya pia tunapokea na kuwapatia huduma stahili," amesema Mkwama.
Mmoja wa wananchi waliopatiwa msaada huo, Hamida Ramadhani ameishukuru LHRC na wadau wote wa sheria kwa kuweka kambi katika maeneo hayo, kwani inawasaidia kutatua changamoto zao.
LHRC katika utoaji msaada huo wanasaidiana na Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Mfuko unaotoa msaada wa huduma za kisheria (LSF).