Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatenga mabilioni kununua vifaa vya hospitali

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imetenga Sh33.5 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba katika hospitali za halmashauri 67 nchini.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imetenga Sh33.5 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa ajili ya hospitali 67 za halmashauri nchini.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Februari 9, 2021 na naibu waziri wa Tamisemi,  Dk Festo Ndugange leo Jumanne Februari 9, 2021 wakati akijibu swali la mbunge wa Mbogwe (CCM),  Nicodemus Maganga.

Maganga katika swali lake la nyongeza amehoji ni lini Serikali itapeleka vifaa vya upimaji ikiwemo X- ray na vingine katika hospitali ya wilaya ya Mbogwe.

Akijibu swali hilo Dk Ndugange amesema Serikali imetenga Sh33.5 bilioni kwa ajili ya hospitali 67 za  halmashauri ambapo Mbogwe ni miongoni mwa hospitali hizo.