Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaunda bodi mshahara kima cha chini

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2022/2023 leo Jumatano Aprili 2022. Picha na Said Khamis

Muktasari:

Serikali imeunda bodi ya kutafakari kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi ambayo itafanya utafiti na kutoa ushauri wa namna ya utekelezaji.

Dodoma. Serikali imeunda bodi ya kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi ambayo itafanya utafiti na kutoa ushauri.

 Hayo yamesemwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2022/2023.

Profesa Ndalichako amesema Serikali imeunda bodi ya kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi ambayo ameizindua juzi.

“Nitumie fursa hii kuwasihi waajiri wote nchini pamoja na wafanyakazi kutoa ushirikiano katika bodi hii ili iweze kufanya kazi yake iweze kufanya utafiti na kutoa ushauri kwa serikali juu ya kima cha chini cha mishahara,”amesema.

Kuhusu mabaraza ya wafanyakazi, Profesa Ndalichako amewasihi waajiri nchini kuhakikisha mabaraza hayo yanaundwa na yanafanya kazi.

“Mabaraza haya ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna kuwa na maelewano baina yao na kutatua migoro ambayo itakuwa imejitokeza,”amesema.

Aidha, amekiri kuwa ni kweli baadhi ya wastaafu wamekuwa wakichelewa kulipwa mafao yao na wengine wakipata usumbufu wa kupeleka nyaraka mbalimbali.

Amesema Serikali inalifanyia kazi kwa kuboresha mifumo ya Tehama na kwamba changamoto inayojitokeza watu walioajiriwa kabla ya mifumo hiyo kuwa imara kumbukumbu zao zilikuwa zinatunzwa katika nakala ngumu.

Hata hivyo, amesema kuwa wanafanyia kazi jambo hilo na kuhakikisha kuwa wanaoondoa hiyo kero inayowakabili hasa wafanyakazi walioingia katika mifuko hiyo kabla yam waka 1999.