Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh31 bilioni kupambana na maji kwenye makazi ya watu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Reuben Kwagilwa wakati akijibu maswali ya wabunge leo Mei 6, 2026 bungeni Dodoma

Muktasari:

  • Katika mpango huo, upande wa Zanzibar peke imeonekana kuwa na maeneo 148 yaliyo kwenye hatari ya kuharibika na tayari halmashauri 11 zimeingizwa katika mradi huo.

Dodoma. Serikali imetenga jumla ya Sh31 bilioni kwa ajili ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi awamu ya kwanza ili kujenga maeneo yaliyoanza kuharibika na kufanya maji ya bahari kuingia katika makazi ya watu.

Katika mpango huo, upande wa Zanzibar peke imeonekana kuwa na maeneo 148 yaliyo kwenye hatari ya kuharibika na tayari halmashauri 11 zimeingizwa katika mradi huo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Reuben Kwagilwa ameliambia Bunge leo Jumatano, Mei 6, 2026 ambapo amesema chanzo cha tatizo hilo ni mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Nungwi (CCM), Mdowe Haji Kombo ambaye ameuliza ni lini Serikali itajenga ukuta katika Fukwe za Bahari ya Nungwi Kiungani ili kuzuia bahari kuingia katika makazi ya watu.

Katika swali la nyongeza Mbunge huyo amehoji majibu ya Serikali yasiyobadilika kwamba tangu katika bajeti ya 2023 yamekuwa ni majibu yaleyale.

Naibu Waziri amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ametaja baadhi ya hatua hizo ni kupambana na mmomonyoko wa fukwe unaosababisha bahari kuingia katika makazi ya wananchi.

“Katika kutekeleza hili, Serikali imefanikiwa kupata ufadhili kupitia Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund - GCF), ambapo jumla ya Dola za Marekani 500,000 sawa na takribani Sh1.3 bilioni za Kitanzania zimetolewa na mfuko husika kwa ajili ya kutekeleza mradi,” amesema Nhamanilo.

Amesema katika mwaka wa Fedha 2025/26 na 2026/27 wa kuimarisha utayari wa Kisiwa cha Zanzibar ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi ambapo mradi huo utaanza mara baada ya tathmini ya athari hizo kukamilika.