Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh4 bilioni zatengwa ujenzi mahakama ya Afrika

Sh4 bilioni zatengwa ujenzi mahakama ya Afrika

Arusha. Serikali imetenga Sh4 bilioni  kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu ya Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu jijini Arusha.

Mahakama hiyo yenye kiti chake cha kudumu jijini Arusha kwa sasa inafanya shughuli zake katika ofisi  za muda zilizopo katika majengo ya Hifadhi za Taifa(Tanapa).

Akizungumza na waandishi  wa habari katika mahakama hiyo, rais wa mahakama hiyo,  Jaji Imani Daud Aboud ameipongeza serikali kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya ya mahakama.

"Hatua hii ni ya kihistoria na tunatazamia ujenzi wake kuwa wa haraka na ni dhahiri kuwa dhamira ya Tanzania katika kupigania haki za binadamu na uungwaji wake wa mkono usiokuwa na shaka kwa malengo ya muungano wa Afrika," amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema Serikali ya Tanzania imetenga takribani hekta 25 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya mahakama hiyo ambapo yatajengwa eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.


Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na haki za watu ni mahakama iliyoanzishwa na nchi za kiafrika ili kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na watu katika Afrika.

Ilianza shughuli zake rasmi  2006 mjini Addis Ababa na baada ya mwaka mmoja ikahamia kwenye kiti chake cha kudumu jijini Arusha, mahakama hiyo inaundwa na majaji 11, raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.