Shahidi kesi ya Mbowe aeleza alivyoshinda njaa siku kumi polisi

Shahidi kesi ya Mbowe aeleza alivyoshinda njaa siku kumi polisi

Muktasari:

  • Mohamed Ling'wenya, shahidi wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe¬† na wenzake amedai hakula chakula siku kumi akiwa katika kituo cha polisi Mbweni.

Dar es Salaam. Mohamed Ling'wenya, shahidi wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  na wenzake amedai hakula chakula siku kumi akiwa katika kituo cha polisi Mbweni.

Shahidi huyo amedai alifikishwa kituo cha polisi Mbweni Agosti 9, 2020 hadi Agosti 19, 2020 alipofikishwa mahakama ya Kisutu ndipo alikula ugali na dagaa.

Ling'wenya ametoa madai yake leo Jumanne Septemba 27, 2021 katika mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo ndogo.