Shehena ya sigara bandia yakamatwa Shinyanga

Muktasari:

Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba Tanzania (TMDA) kanda ya ziwa magharibi imekamata makasha 2200 ya sigara bandia zilizokuwa zimeingizwa nchini zikitokea DRC Kongo.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba Tanzania (TMDA) kanda ya ziwa magharibi, imekamata shehena ya sigara bandia aina ya SuperMatch yenye thamani ya Sh1.8 bilioni.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 28, 2022 na Meneja wa kitengo cha Uhusiano TMDA, Gaudensia Simwanza imeeleza walipokea taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Shinyanga.


“TMDA kanda ya ziwa magharibi  baada ya kupokea taarifa ya kontena lenye bidhaa za tumbaku lililozuiliwa katika ofisi ya TRA Shinyanga, imebaini sigara hizo ni bandia na zimeingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Kongo ambapo kuna makasha 2200 yenye thamani ya Sh1.8 bilioni.
“Makasha hayo yana uzito wa tani 13.2 kazi hii tulishirikiana kwa karibu sana na MCIE, lakini cha kujiuliza zimepitaje mipakani na tunao wakaguzi huko? Hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na mzigo huu umezuiliwa,” amesema Simwanza.