Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheikh Walid ataka waumini kuendeleza matendo mema hata baada ya mfungo

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam leo Ijumaa.

Muktasari:

Waislamu duniani kote hivi sasa wamo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Dar es Salaam. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omari ametoa wito kwa Waislam wote nchini kuendelea kutenda matendo yaliyomema hata wakiwa nje ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sheikh Walid ameyasema hayo leo, katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Waislam wote kujifunza maisha waliyonayo ndani ya Mwezi wa Ramadhani na waishi hivyo hivyo siku zote.

“Katika Mwezi wa Ramadhani Waislam wote wanatakiwa wamuoneshe asiyekuwa Muislam kwamba, uonekane ukarimu wake, huruma na huzuni yake, mpaka  aiyekuwa Muislam atamani kuwa Muislam ’’amesema Sheikh Walid.

Amesisitiza pia kuwa dini ya Kiislam sio dini ya dini ya kigaidi wala ya kuua watu bali dini hiyo ni dini ya amani na kutenda mema kwa watu wote hata wasiokuwa Waislam.

“Si ajabu kuwa utasikia watu huko wakisema kuwa Uislam ni dini ya kigaidi kazi yake ni kuua watu la, Uislam siyo dini ya kigaidi kwani ninavyowaona Waislam ndani ya Mwezi wa Ramadhani ndivyo walivyo’’ amefafanua Sheikh Walid.

Pamoja na hayo, ameongeza kuwa wanazuoni waliopita wote wamesema kuwa Mwezi wa Ramadhani ni Mwezi wa kimapinduzi na ni mwezi wa kuwageuza watu fikra na kuwarudisha watu wote katika Uislam.