Waislamu wapewa neno mwezi wa Ramadhani

Muktasari:
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum amesema yatafanyika mashindano ya kuhifadhi Quran
Dar es Salaam.Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kutenda haki na kujiepusha na mambo yasiofaa katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Mei 17, 2018 na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum, ikiwa ni siku ya kwanza tangu kuanza kwa mfungo.
Amewataka Waislamu wote matendo yao yaendane na mfungo, “Katika mwezi huu unatakiwa kufunga mikono yako isichukue rushwa, riba, haki ya mtu pamoja na kuchunga mipaka yako na usiende sehemu zenye matendo haramu.”
Ameongeza kuwa Serikali imefanya jitihada katika kipindi hiki cha mfungo kutokuwa na shida ya sukari pamoja na mafuta.
Amesema yatafanyika mashindano ya kuhifadhi Quran ambayo yataanza Mei 20, 2018 katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
“Katika kipindi hiki cha mfungo tumeandaa yatakayofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ukumbi wa PTA na kuendelea Mei 26 na 27 kwenye viwanja vya mnazi mmoja,” amesema.