Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shikuhata wataka safari za usiku zisitishwe

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Shirika la Kupambania Haki za Abiria Nchini (Shikuhata), Ambakisye Mwakifwange ameshauri Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kusitisha huduma za usafiri wa mabasi yaendayo mikoani kutokana na changamoto sita ikiwamo ushahidi wa siku chache za majaribio.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Shirika la Kupambania Haki za Abiria Nchini (Shikuhata) Ambakise Mwakifwange ameshauri Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kusitisha huduma za usafiri wa mabasi yaendayo mikoani kutokana na changamoto sita, ikiwamo ushahidi wa siku chache za majaribio.

Mwakifwange ametoa kauli hiyo leo Julai 5, 2023 wakati wa mjadala kuhusu uamuzi wa Serikali kuruhusu mabasi kufanya safari saa 24 kupitia Jukwaa la Mwananchi Twitter space linalofanyika kila Jumatano chini ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Akitoa hoja ya kuahirisha vikao vya Bunge Juni 28, mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza rasmi kuondoa zuio la safari za usiku lililokuwepo tangu Mwaka 1992.

Katika mjadala huo, Mwakifwange amesema ndani ya siku chache baada ya kurejea huduma hizo, tayari ajali tatu zimetoa usiku za mabasi huku Latra ikikiri madereva kukimbia kusikojulikana bila kufahamika majina yao.

“Kama ajali tatu ndani ya wiki moja, je itakuwaje kwa mwezi mmoja? Watu wangapi wanapoteza maisha na tunawezaje kudhibiti safari za usiku? Tulishauri basi moja liwe na madereva wawili ili kupokezana lakini haikutekelezwa,” amesema Mwakifenga.

Pili, Mwakifwange ameshauri kusitishwa huduma hiyo usiku kutokana na tabia za madereva kutumia vilevi bila kudhibitiwa na kwamba usiku watakuwa huru zaidi hatua itakayohatarisha usalama wa abiria.

Tatu amesema safari za usiku pia zinahatarisha usalama wa abiria kutokana na changamoto za usafiri wa bodaboda na bajaji wanapoelekea vituoni kusafiri pamoja na tishio la matukio ya utekaji wa mabasi njiani.

“Pia, barabara zetu bado nyembamba kwa kupishana hivyo usiku ni hatari zaidi na maeneo mengine zimelika kingo pembeni kwa hiyo wakati wa kupishana ni hatari, maeneo mengi pia hakuna alama kusaidia na matuta hayana alama kwa hiyo wanapanda tu,”amesema Mwakifwange.

Katika ufafanuzi wake, Mwakifwange amesema hatari zaidi majeruhi wa ajali wakati wa usiku sio rahisi kupata msaada wa haraka badala yake vibaka wanavamia kupora.

“Lakini pia usiku polisi pia wachache kutoa huduma, kwa hiyo sisi hatupingani na Serikali lakini tunaona bado hatujajipanga kama Taifa, kwa nini tuendelee kuwa Taifa lenye ajali mbaya duniani?