Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sifa mbaya, nzuri kwa mwanamke wa ndoa hizi hapa

Baadhi ya washiriki katika kongamano la Wanaume wakimsikiliza Sheikh Ibrahim Bombo (hayupo pichani) wakati wa kongamano hilo jijinj Mbeya.

Muktasari:

Sheikh huyo amesema zipo sifa saba ambazo hazifai kwa mwanamke wa kuwa naye kwenye ndoa au kwenye uhusiano, huku akiitaja sifa nyingine nne za mke bora na mwema.

Mbeya. "Kama umeoa au upo kwenye uhusiano na mwanamke mwenye sifa mojawapo kati hizi omba ushauri au achana naye."

 Ni kauli ya Imamu wa msikiti wa Al Baraa Ibn Azib Mbeya, Sheikh Ibrahim Bombo wakati wa kongamano la Wanaume lenye kauli mbiu ya 'Bro...Funguka' lililofanyika leo Jumapili, Novemba 20, 2022 jijini Mbeya.


Kauli hiyo imetolewa baada ya baadhi ya wanaume 'kufunguka' mazito wanayopitia kwenye familia zao bila kutoa taarifa wakidai kudharauliwa au kufedheheshwa na jamii inayowazunguka.


Bombo ametaja sifa tano kati ya saba ambazo mwanamke akiwa nazo hafai kuolewa au kuwa katika uhusiano na mwanamume kama vitabu tukufu vinavyoelekeza.


Ametaja sifa hizo kuwa kulalamika, kudhihaki akifafanua mwanamke yeyote anayelalamika kila wakati kwa mume wake hafai.


Amesema sifa nyingine ni kushtaki kila kitu, majivuno, tamaa na kutoridhika huku suala la haki ya ndoa kuwa na sababu nyingi ikiwamo kuumwa, au mabadiliko ya mwili huyo hafai.



"Zipo sifa saba mbaya za mwanamke, muda wote anasema yeye ni mzuri hivyo wewe siyo wa aina yake, anapenda sana kwenda na wakati bila kujua au kujali kipato na uwezo wa mume wake na muda mwingine anakulinganisha na wapenzi wake wa zamani au maisha ya nyumbani kwao, muda wa tendo la ndoa anakuwa na sababu nyingi sasa wa aina hiyo achana naye au omba ushauri," amesema Bombo.


Sheikh huyo ametaja pia sifa za mwanamke anayepaswa kuolewa kuwa ni uzuri wa sura na umbo kwa ujumla, uchumi wake, hali ya ukoo wake na maadili au heshima kujua mipaka yake kwa mume wake.


Kwa upande wake, mmoja wa wanaume aliyeshiriki kongamano hilo, Anyimike Hezron amesema licha ya wanaume kuwa na wajibu wa kutunza familia, lakini baadhi ya wanawake hasa wenye kazi hawatimizi wajibu na haki kwa wanaume.


"Mwanamume utaleta matumizi yote lakini utapokelewa na dada wa kazi, muda mwingine hata ile haki ya ndoa hupewi ukiuliza anasema amechoka, hivyo kwenda kuongea kwenye jamii inakuwa ngumu," amesema Hezron.


Naye Alex John amesema ni bora kuwapo maboresho ya sheria kwani nyingi zinambeba mwanamke na watoto katika ishu ya ukatili wa kijinsia.


"Hata ile sheria ya mwaka 1971 ya kwamba mwanamke anaweza kukopa kwa dhamana ya mwanamume ni ukatili, atakopaje bila kunishirikisha au kujua uwezo wangu kiuchumi? Naona kuna haja ya maboresho ili na sisi wanaume tupewe haki," amesema


Mkurugenzi wa shirika la Empower Youth Prosperity (EYP), Ipyana Mwakyusa amesema mkakati wao ni kuhakikisha wanaifikisha program hii kitaifa ili kuwaamsha wanaume kufunguka ukatili wanaokutana nao.


"Tunatarajia kongamano hili liwe la kitaifa ambapo tutaandaa kwa kuwashirikisha wanaume wote nchini tujadili na kuazimia," amesema Mwakyusa.


Afisa Tarafa Usongwe mkoani hapa, Ildephonce Kamugisha amesema mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kila kata inakuwa na afisa ustawi ili kuchukua changamoto za wananchi bila kubagua jinsia.


"Lakini pia kumekuwa na tatizo kwa baadhi ya watumishi kutoa taarifa za wateja wao kuzipeleka vijiweni, tunaendelea kuwafuatilia na watakaobainika tutawachukulia hatua kali," amesema Kamugisha.