Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri yafichuka wanaume zaidi kutahiriwa wilayani Kahama

Siri yafichuka wanaume zaidi kutahiriwa wilayani Kahama

Muktasari:

  •  Imeelezwa kuwa baadhi ya wanawake wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuwanyima unyumba waume zao kushinikiza wafanye tohara kwa ajili ya kujikinga na maambukizi  ya VVU na saratani ya shingo ya mlango wa kizazi,  kumeongeza idadi ya wanaume wanaotaka kutahiriwa.

  

Kahama. Imeelezwa kuwa baadhi ya wanawake wilayani Kahama mkoani Shinyanga kuwanyima unyumba waume zao kushinikiza wafanye tohara kwa ajili ya kujikinga na maambukizi  ya VVU na saratani ya shingo ya mlango wa kizazi,  kumeongeza idadi ya wanaume wanaotaka kutahiriwa.

Hayo yameelezwa na mratibu wa tohara manispaa ya Kahama,   Hadji Sued  leo Alhamisi  Agosti  19,  2021 katika mkutano wake na wanahabari kwenye eneo la utoaji wa huduma ya tohara akibainisha kuwa baada ya mkakati huo wa wanawake, idadi ya wanaume wanaojitokeza kufanyiwa tohara inazidi kuongezeka kila siku.

Amesema wajawazito wamechukua hatua hiyo baada ya kupewa elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na watoa huduma wafikapo kliniki kupata huduma ya afya ya uzazi.

Sued amesema kuanzia Januari hadi Julai 2021  wamewatahiri  wanaume  335 na mwaka  2020 kuanzia Oktoba  hadi Desemba walitoa huduma hiyo kwa zaidi ya wanaume 400.

Amesema mwaka 2020  waliweka malengo ya kutoa huduma ya tohara kwa watu  6,755 na walifika lengo na mwaka 2021  kuanzia Septemba wanatarajia kutoa huduma hiyo kwa vijana,  watu wazima na wazee 14,000 ambapo kila mwezi watakuwa wanawafanyia tohara watu  1,170.

Sued amesema utoaji wa huduma hiyo imesaidia kupunguza wimbi la maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa asilimia 5.3 ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo ilikuwa asilimia 6.4.

Amesema mwaka 2010/11 Mkoa wa Shinyanga ulikuwa juu kwa maambukizi ya VVU kwa asilimia 7.4 na mwaka 2015/16 maambukizi yalipungua kwa asilimia 5.9.

Lukia Abdallah aliyefika katika hospitali ya manispaa amesema elimu ya tohara aliipata tangu akiwa anasoma elimu ya dini hivyo watoto wake wa kiume wote wamefanyiwa tohara.

Mwanamke mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina ameieleza Mwananchi Digital kuwa wakati anampeleka mwanaye  kufanyiwa tohara aliambatana na mumewe ambaye alikuwa hajafanyiwa tohara na siku ambayo alimfanyia tohara mwanaye na mumewe naye alifanyiwa.