Spika Ndugai amuonya Nape kuhusu wabunge 19 Chadema

Monday May 03 2021
By Habel Chidawali

Dodoma. Spika wa Bunge,  Job Ndugai amemuonya mbunge wa Mtama (CCM),  Nape Nnauye kuchunga kauli zake anapochangia kuhusu masuala ya wanawake.

Ametoa onyo hilo leo Jumatatu Mei 3,  2021 alipozungumzia  mchango wa mbunge huyo kuhusu wabunge 19 ambao Chadema imetangaza kuwafukuza uanachama na ambao bado wameendelea kuwa wawakilishi wa chama hicho bungeni.

Hivi karibuni Nape akiwa kwenye mjadala nje ya Bunge alikosoa wabunge hao kuendelea kuwepo bungeni licha ya kufukuzwa Chadema, huku akitaka Katiba ya nchi ifuatwe.

Nape pc

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza bungeni kuhusu kuendelea kutambuliwa kwa wabunge 19 wa Viti Maalumu wa Chadema bungeni alipokuwa akiongoza kikao cha Bunge jijini Dodoma leo. Kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akimsikiliza spika. Picha na Edwin Mjwahuzi

"Hivi karibuni mbunge wa Mtama mdogo wangu Nape Nnauye alitoa mchango wake hapa, Sina haja ya kuzuia uchangiaji wake lakini alikiuka kanuni kwa kuwataja wabunge kwa majina, hapo alikosea sana," amesema Spika Ndugai.

Advertisement