Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TADB kuwapa wavuvi zana

Muktasari:

  • Wavuvi wanaofanya uvuvi wa mazao ya bahari wanatarajia kunufaika baada ya kupatiwa mikopo ya zana za uvuvi ili kuboresha shughuli za uvuvi.

Morogoro. Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa mikopo yenye thamani ya Sh25.175 bilioni kwa wavuvi wadogo kwa lengo la kuongeza kasi ya uzalishaji wenye tija.

Hayo yameelezwa leo na Ofisa Maendeleo ya Biashara wa banki hiyo, Angelina Nyansaambo leo Oktoba 12 wakati mafunzo kwa maofisa uvuvi kutoka kwenye halmashauri tano za Mkoa wa Pwani zenye ukanda wa bahari kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. 

Amesema benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa maofisa hao ili wakawafundishe wavuvi wadogo namna ya uvunaji wa mazao ya bahari.

“Tumetoa mikopo kwa mvuvi mmoja mmoja na vikundi na hitaji letu ni kuhakikisha wavuvi wanafikiwa ili waweze kusimamia biashara zao na kuhudumia mikopo.

“Tunategemea kutoa mikopo kwa masharti nafuu, lakini kabla ya kuwapa tutawajengea nuwezo wa ujasiliamali na usimamizi wa fedha, ndipo yanapokuja mafunzo maofisa uvuvi wa Wizara ili watakapoenda huko wawe na uelewa na kuwafundisha wavuvi wadogo,” amesema.

Amesema mpaka sasa benki hiyo imefanikiwa kutoa boti 33 ili kusaidia wavuvi kujikwamua kiuchumi.

Akizungumzia mafunzo hayo, ofisa uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sikudhani Mponda amesema Wizara ya wanatekeleza progaramu ya kuendeleza kilimo na uvuvi (ASDP) inayofadhiliwana Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ambapo lengo lake ni kuwainua wavuvi kiuchumi.

“Kwa upande wetu sekta ya uvuvi programu inatekelezwa katika halmshauri sita, lakini kwa sasa tumeanza nazo nne ambazo ni Pangani, Bagamoyo, Kilwa na Mafia,” amesema.

Naye mteknolojia wa samaki mwandamizi wa wizara hiyo, Masui Munda amesema mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa namna ya kutoa elimu kwa jamii ya wavuvi katika mnyororo wake kwa kujaribu kuwabadirisha kufanya shughuli zao kwa mtazamo wa kibiashara.