Tambwe Hiza: Tushindane kwa hoja

Muktasari:
Alisema kukishakua na figisufigisu ndio hapo vurugu zinapoanza kutokea jambo ambalo chama chao kisingependa yatokee.
Kada wa Chadema, Tambwe Hiza amesema watu wanapaswa kujua uchaguzi sio vita, na kila mmoja anapaswa kushindana kwa haki.
Alisema kukishakua na figisufigisu ndio hapo vurugu zinapoanza kutokea jambo ambalo chama chao kisingependa yatokee.
Pia Hiza kaonya watu wa Serikali kutowatisha wananchi kwa sababu wao ndio wamewachagua na kuwaweka madarakani.
Kada huyo amesema wakati CCM wakisema Salum Mwalimu Mzanzibar mbona hawamsemi Mtulia ambaye ni Mpemba.
"Tunataka wajue hatujaja kushindana hapa kwa makabila wala udini bali tumekuja kushindana kwa hoja za chama kipi bora na wanaochagua wanachagua ubora wa mgombea na sio dini wala kabila lake," amesema Hiza.
"Tunapokuja kwenye kampeni tuangalie mambo ya msingi, na sio ya mtu kusimama na kusema nampenda mtu fulani wakati kuna mamilioni ya wananchi Kinondoni waliokuamini na kuchagua utawaondolea matatizo yanayowakabili," alisema Kada huyo.
Serikali nzima imeshindwa na Bakhresa ambaye anamiliki kiwanda cha unga, meli, sasa kuliko kuichagua CCM si bora kumchagua Bakhresa na kueleza kwamba wasipowachagua Chadema hawawakomoi wanachama wa chama hicho bali wanajioa na wao.