Tamwa yaiomba Serikali kutumia majadiliano Loliondo

Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Dk Rose Reuben

Muktasari:

Chama cha Habari Wanawake nchini (Tamwa) kimeiomba Serikali kutumia mbinu ya majadiliano na maridhiano katika taratibu za uhamishaji unaohusisha ardhi na raslimali za taifa.

Dar es Salaam. Chama cha Habari Wanawake nchini (Tamwa) kimeiomba Serikali kutumia mbinu ya majadiliano na maridhiano katika taratibu za uhamishaji unaohusisha ardhi na raslimali za taifa.

Ombi hilo limakuja baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii za wafugaji wa kabila la Maasai wa Loliondo na vikosi vya askari wakipingana utekelezwaji wa kuwekwa alama za mipaka kwa kumegua kilometa za mraba 1500 za vijiji vyao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Juni 10/2022 na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Dk Rose Reuben imeeleza kuwa wanafahamu na kukubalina na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba kupotea kwa amani katika eneo lolote kunasababisha usumbufu kwa wanawake, wazee na watoto .

“Na hiyo tunaitaka kurejea meza ya majadiliano ili kumaliza mgogoro wa uhifadhi wa maeneo ya Loliondo na jamii ya kimasaai,”aimeeleza taarifa hiyo

Taarifa hiyo imefafanua kuwa taasisi hiyo imeshuhudia migogoro mingi ikitatuiliwa kwa njia ya mazungumzo na maridhiano hapa nchini, hivyo wanaamini hata mgogoro huo pia unaweza kumalizika bila kutumia nguvu wala kuzusha taharuki inayolipaka taifa matope ya uvunjifu wa haki za binadamu.