Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tasaf yafikia walengwa vijiji 115 Misungwi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene (wakwanza kushoto) akikagua ujenzi wa shule maalum ya wasichana inayojengwa na Tasaf katika Kata ya Mabuki wilayani Misungwi. Picha na Saada Amir

Muktasari:

Mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) umetoa ruzuku kwa walengwa 12, 466 wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza yenye thamani ya Sh6.5 bilioni kwa awamu 15 kuanzia 2020 hadi Julai 2023.

Mwanza. Mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) umetoa ruzuku kwa walengwa 12, 466 wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza yenye thamani ya Sh6.5 bilioni kwa awamu 15 kuanzia 2020 hadi Julai 2023.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Tasaf wilayani humo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene leo Ijumaa Agosti 4, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Joseph Mafuru amesema  hadi sasa mpango huo umetoa ruzuku kwa wakazi wa vijiji 115.

“Mpango umefanya utambuzi kwenye kaya zenye walemavu, kuwaandikisha na kutoa ruzuku ambapo jumla ya idadi ya kaya zilizofikiwa hadi sasa 13,205 kati ya hizo kaya 1,932 zilipitishwa na jamii na kaya 1,740 zilikubaliwa na sasa zinapata ruzuku,

“Katika awamu ya Tasaf wilaya imepokea jumla ya zaidi ya Sh21 bilioni, mpaka sasa miradi 358 yenye thamani ya Sh3.73 bilioni imetekelezwa huku, vikundi 892 vya kuweka akiba na kutunza uchumi wa kaya vimeundwa  katika vijiji 115 ambavyo vimepatiwa nyaraka za utunzaji kumbukumbu, mafunzo ya viongozi na vyote vikisajiliwa kwa mfumo wa Tasaf na vikundi 703 vimesajiliwa katika mfumo wa Benki Kuu,”amesema

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ametembelea na kukagua ujenzi wa shule maalum ya wasichana inayojengwa na Tasaf katika Kata ya Mabuki, ambayo itawanufaisha wanafunzi wa kike katika vijiji vya Mwanangwa, Mwagagala, Lubuga, Mhungwe na Ndinga.

Mratibu wa Tasaf wilayani humo, Gloria Buname amesema ujenzi huo  ulianza Aprili, 2022 na kutarajiwa kukamilika na wanafunzi kuanza kutumia  majengo yake Januari, 2024.

“Awamu ya kwanza ya ujenzi umegharimu Sh648.7 milioni ukihusisha bweni, bwalo la chakula, madarasa manne, ofisi ya walimu na matundu sita ya choo vitakavyokamilika Juni 30, mwaka huu huku, awamu ya pili inayogharimu Sh286.7 ikihusisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu (two in one), jengo la maabara na utawala,”amesema

Amesema kwa sasa wanafunzi wa vijiji hivyo wanategemea Shule ya Sekondari Mawe Matatu iliyopo Kilometa 20 kutoka kijiji cha Mwanangwa nakudai ujenzi huo utakapokamilika utachukua wanafunzi 400 ikianza na 200 huku, bweni likiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 160 ambapo itaanza na wanafunzi 80.

Akizungumzia ujenzi huo, Simbachawene amewaagiza Tasaf kwa kushirikiana na Halmashauri ya Misungwi kujenga wigo kwenye shule hiyo pamoja na njia za kupita wanafunzi kutoka Jengo moja kwenda jingine ili maeneo ya shule yawe nadhifu.