Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TBA: Ikulu Chamwino kuongeza ya wananchi kwa Serikali

Muktasari:

  • Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi huo ilifanyika Mei 30, 2020, tukio ambalo lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majenzi Tanzania (TBA), Daud Kondoro amesema kukamilika kwa ujenzi wa Ikulu ya Dodoma kumeongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao ambayo kwa miaka mingi iliahidi kuhamia Dodoma.

 Kondoro amebainisha hayo leo Mei 20, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma ambayo itakuwa ni ofisi pamoja na makazi rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema ujenzi wa Ikulu ya Dodoma unafuatia uamuzi wa Serikali wa kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma uliotolewa Julai 23, 2016 na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.

“Ujenzi huo umeongeza Imani ya wananchi kwa serikali yao kwa kutimiza ahadi ya kuhamia Dodoma. Pia, imeongeza ukuaji wa maeneo yanayozunguka ikulu ya Dodoma,” amesema Kondoro.

Kondoro amesema utekelezaji wa ujenzi huo ulianza ikiwemo upanuzi wa Ikulu ya Chamwino ambapo eneo la Ikulu liliongezwa kutoka ekari 66 zilizokuwepo tangu awali hadi ekari 8,473 baada ya kutwaa maeneo mengine ya jirani.

Ili kuharakisha mchakato wa ujenzi wa ikulu, amesema TBA iliharakisha ujenzi wa jengo la ofisi za muda ikiwemo jengo la utawala, jengo la makazi ya Rais pamoja na majengo mengine saidizi ambayo ni uhasibu, ununuzi, ugavi, karakana, zahanati na kituo cha mafuta

Pia, amesema ujenzi huo ulihusisha ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo lote la ikulu ya chamwino. Majengo yote hayo, amesema ni ubunifu wake umefanywa na TBA lakini yamejengwa kwa kushirikiana na Suma JKT.

“Makabidhiano ya eneo la ujenzi na mkandarasi Suma JKT yalifanyika Januari 21, 2020 ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na makatibu wakuu kutoka ofisi ya rais, Wizara ya Ujenzi pamoja na mkuu wa JKT,” amesema.

Mtendaji huyo wa TBA amesema ujenzi huo ulifanyika kwa mfumo wa operesheni maalumu ambapo Ofisi ya Rais Ikulu kama mshitiri akifuatilia kwa karibu na kutoa uamuzi wa ujenzi huo,

Ameongeza kwamba hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi huo ilifanyika Mei 30, 2020, tukio ambalo lilihushuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu.

“Wataalamu walihakikisha kwamba wanapata vipimo sahihi na kuhakikisha kwamba jengo la Dodoma linakuwa na mfanano na lile la Dar es Salaam,” amesema Kondoro.