Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TBS yazidi kueleza kuhusu hatua dhidi ya mafuta ya Oki

Muktasari:

  • Ni baada ya kutangaza kwamba mafuta ya Oki na Viking  hayafai, sasa yasema yanayotengenezwa nchini safi

Dar es Salaam. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekiri kukabiliwa na  changamoto ya kuwadhibiti wauzaji wa mafuta ya kula kwa kipimo, katika utekelezaji  wa kuzuia matumizi ya mafuta ya Oki, Viking na Asma.

Ofisa Mkaguzi wa TBS, Lazaro Msasalaga alisema kuwa hatua hiyo inatokana na kwamba ni rahisi kwa wanunuzi wa mafuta hayo kwa jumla kuepuka kununua mafuta ambayo alifafanua kuwa yanaingizwa nchini kwa njia za maficho.

“ Sisi tunawataka wananchi kuwa makini kwa kuangalia kwenye nembo mafuta ya aina hizo tulizotaja yanayotengenezwa hapa nchini ni salama na yana nembo yetu lakini hayo tuliyoeleza hayafai kwa matumizi yanatoka nje ya nchi na hayana nembo yetu, tunajua ni vigumu kwa wanaonunua kwa vipimo kusoma  nembo, lakini pia wauzaji wanaweza kubadilisha ndoo, hii ni changamoto,” alisema.

Msasalaga alisema kuwa mafuta hayo hayana ubora wa kiwango chenye namba TZS 559 Palm olein specification, ingawa hakina madhara ya moja kwa moja kwa mtumiaji lakini kina umuhimu kwa bidhaa hiyo.

Wakati huohuo TBS imeufungia mgahawa wa Yami Yami iliyopo eneo la Posta jijini Dar es Salaam,  unaozalisha mikate na vitafunwa, kuendelea kuzalisha bidhaa hivyo baada ya kutosajiliwa.

Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile alisema kuwa hatua hiyo inatokana na wamiliki wa mgahawa huo kutoitikia wito wa kupeleka bidhaa zao kukaguliwa kama zina ubora wa kiwango cha lazima kinachohitajika kwenye bidhaa hizo.

Hatua hiyo iliwashtua wafanyakazi wa mgahawa huo ambapo Ofisa Uhusiano wao, aliyejitambulisha kwa jina la Fatma Omary alipinga  na kujaribu kuzuia maofisa wa TBS kuitekeleza.

“Hii siyo busara mbona hatuna taarifa yoyote ya ujio wenu mahali hapa, mnatuvamia na kutushtukiza, tutafungaje nasi tunazalisha mikate mizuri na tunazingatia ubora , pia nimeambiwa na viongozi wangu kuwa tupo kwenye mchakato wa kusajili huko TBS,” alilalamika ofisa huyo.

Mwanasheria wa TBS, Baptister Bitaho alisisitiza kufunga uzalishaji huo, akieleza kuwa wametoa matangazo kwenye vyombo vya habari miezi miwili ilivyopita wakihamasisha watengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazoangukia kwenye viwango wafike ,lakini hawakuitikia wito huo.

Naye mwanasheria wa mgahawa huo Said Issale alikubaliana na hatua hiyo akieleza kuwa ni utekelezaji unaofanywa kwa kuzingatia sheria ambayo inalenga kusimamia uzalishaji wa bidhaa zenye viwango nchini, hivyo aliwashauri wateja wake kufunga na kufuatilia utaratibu wa kujisajili kwa mujibu wa sheria.