Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TCRA yaifungia Wasafi TV miezi sita

Muktasari:

TCRA imesema Wasafi TV walikiuka kanuni za utangazaji katika tamasha la ‘Tumewasha na Tigo.’

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa miezi sita kituo cha teloevisheni cha Wasafi kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji katika matangazo yake ya moja kwa moja ya tamasha la ‘Tumewasha na Tigo’.
 Uamuzi huo umefikiwa leo Jumanne Januari 5 baada mamlaka hiyo kukutana na uongozi wa Wasafi TV na kusikiliza utetezi wao.
Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Johanes Kalungule amesema ukiukwaji huo ulifanyika Januari 1, 2021 ambapo televisheni hiyo ilirusha maudhui yaliyomuonyesha msanii Gigy Money akicheza katika mitindo iliyoonyesha utupu wake.
Kalungule amesema kosa hilo ni kinyume na kanuni za utangazaji, hivyo kuanzia muda uliotolewa uamuzi huo Wasafi TV imetakiwa kusitisha matangazo yake na kuomba radhi mfululizo.
“Pia TCRA imesitisha utoaji wa huduma za utangazaji za Wasafi TV kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari 6, 2021 hadi Julai 6.
Amesema iwapo Wasafi Tv itakaidi uamuzi huo hatua zaidi za kisheria na za kiuthibiti zitachukuliwa dhidi yao.