Tendega adai aliitwa kuhojiwa kwa Whatsapp njia isiyo sahihi
Mbunge wa viti maalum, Grace Tendega
Muktasari:
- Shahidi wa kwanza upande wa walalamikaji katika kesi ya wabunge 19 wa viti maalim waliofukuzwa uanachama wa Chadema Grace Tendega amehitimisha ushahidi wake pamoja na mambo mengine akisisitiza kuwa waliofukuzwa uanachama bila kupewa haki ya kusikilizwa
Dar es Salaam. Mbunge wa viti maalum ambaye ni mmoja wa wabunge viti maalim 19 waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega ameieleza mahakama alifukuzwa uanachama bila kupewa haki ya kusikilizwa.
Tendega ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema(Bawacha) ametoa maelezo hayo mahakamani leo Alhamis, Oktoba 13, 2022, wakati akihitimisha ushahidi wake katika kesi yao ya kupinga kufukuzwa uanachama wa chama hicho.
Wabunge hao akiwamo Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).
Hata hivyo jopo la mawakili wa Chadema linaloongozwa na Peter Kibatala liliomba mahakama na ikaridhia na kuwaamuru wabunge hao wanane kati yao akiwAmo Mdee wafike mahakamani kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano kuhusiana na ushahidi wao yaani malalamiko yao waliyoyato kwenye viapo vyao.
Shauri hilo namba 36 la mwaka 2022 lilianza kusikilizwa rasmi Ijumaa iliyopita, ambapo Tendega alifungua pazia kwa kuwa wa kwanza kupanda kizimbani na kuwekwa katika kikaango cha maswali kutoka kwa wakili Kibatala.
Leo Alhamisi, Tendega amesema alitumiwa barua ya wito wa kwenda kuhojiwa Kamati Kuu ya Chadema kuhusu tuhuma za kukubali kuapishwa kuwa mbunge wa viti maalum, kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.
Akiihojiwa na Wakili wake Ipilinga Panya, ambaye alikuwa akimuuliza maswali ya kumuongoza kusawazisha na kufafanua Majibu yake aliyoyatoa wakati akihojiwa na Wakili Kibatala, amesema kuwa ingawa Katiba ya Chadema inatambua matumuzi ya Teknolojia ya Habari, katika mawasiliano, lakini Whatsapp haijatajwa isipokuwa barua pepe tu.
Amesema kwa kuwa wakati akiipokea barua hiyo ya Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika Novemba 25, 2020 ikimtaka afike makao makuu ya Chama Dar es Salaam,Novemba 27 kuhojiwa, alikuwa jijni Dodoma na kwamba aliandika barua kuomba aongezewe muda.
Amesema No emba 26, Mnyika alimwandikia barau nyingine ya akimweleza kuwa kikao kingafsnyika katika hotel ya Ledger na kwamba barua hiyo alipata Novemba 27,2020 mchana wakati kikao kilitakiwa kufanyika siku hiyo kuanzia asubuhi.
Kutikana na hali hiyo amesema kuwa alishindwa kuhudhuria ndipo siku hiyo hiyo Kamati Kuu imayoa uamuzi wa kumbuq uanachama.
Pia Tendega alisema kuwa alikata rufaa Baraza Kuu, ambalo lilikaa Mei11,2022 ambako aliitwa lakini pamoja na kuitwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa.
Amesema kuwa badala yake alipewa nafasi ya kuomba radhi na kuoneshwa rufaa yake aithibitishe kama ndio yenyewe kisha akaambiwa atoke njia na baadaye aliitwa na kusomeaa uamuzi wa Baraza Kuu ambalo liliiunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu.
"Sasa mtukufu Jaji una-appologize (unaomba radhi) nini wakati hujasikilizwa.?", amehoji Tendega na kuelezea Katiba na kanuni za Chadema kuhusu .haki za msingi katika kumshughuulikia mwanachama kinidhamu kuwa anapaswa kuelezea tuhuma, na muda wa kuzijibu na kisha kujieleza.
Pia Tendega alisema kuwa hakuweza kuandija barua kumtaka Katibu Mkuu, Mnyika na mwenyekiti,Freeman Mbowe wajiondie kusikilizwa shauri lao kutokana na kuwalalamikia kuwa waliyoa kauli za kuwahukumu kabla ya vikao, kwa kuwa hawakuwa na muda huo, na kwamba biongozi hao wenyewe wanajua misingi hiyo ya Haki lakini waliipuuza.
Baada ya Tendega kuhitimiaha ushahidi wake Sasa ni zamu ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Bawacha Hawa Mwaigunga, kuhojiwa na mawakili wa Chadema kuhusiana na maelezo yake ya kupinga kuvuliwa uanachama aliyoyatoa katika kiapo chake.
bali na na Grace na Mwaifunga wengine walioitwa kuhojiwa ni Halima Mdee, Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, na Cecila Pareso.