Tigo kujisogeza karibu zaidi na wateja
Dar es Salaam. Tigo, Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo hapa nchini imezindua kampeni ya ‘Sako Kwa Bako’ kwa lengo la kuimarisha mahusiano yake na wateja lakini pia kuadhimisha hatua muhimu ya kufikia watumiaji wa huduma zake za simu zaidi ya milioni 20.
‘Sako Kwa Bako’ ni neno linalomaanisha ‘pamoja kila hatua’ lengo lake ni kuonyesha dhamira ya Tigo ya kuboresha uhusiano wake na wateja kwa kuamsha kumbukumbu za thamani za uzoefu wa pamoja, kutoka kauli mbiu za kampeni maarufu hadi bidhaa na huduma zinazobadilisha maisha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo, Kamal Okba alisema, wanasherehekea wateja wetu milioni 20 na kutoa shukrani kwa uaminifu wao usioyumba.
“Safari yetu imekuwa yenye utajiri mkubwa uliojaa uvumbuzi na bidhaa na huduma nyingi za kwanza sokoni pamoja na huduma bora kwa wateja kwa bidii kuhakikisha kila mteja wa Tigo anahisi kuunganishwa, kuthaminiwa, na kuwezeshwa.”
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Isack Nchunda yeye alihusisha ukuaji wa idadi ya wateja na utamaduni wa Tigo unaomlenga mteja, akisema Tigo, imejitosheleza na dhamira yake ya kuongoza mabadiliko ya kidijitali nchini Tanzania.
Nchunda anasema mtandao wa Tigo umepiga hatua kubwa ya kueneza huduma za mtandao wa 4G nchini kote, lakini pia kuanzisha teknolojia ya 5G yenye kasi zaidi katika miji mikuu
“Sako Kwa Bako inaimarisha ahadi ya Tigo ya kutoa huduma na bidhaa bora za kidijitali na kifedha ikikuza kampeni zenye athari kubwa katika kuboresha maisha ya wateja wake kote nchini,” anasema Nchunda.
Aidha uzinduzi kampeni hiyo ni ishara ya hatua ya mtandao huo unaongoza kwa kasi nchini kuelekea kuboresha mawasiliano na uzoefu wa kifedha wa wateja nchini Tanzania.