Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tisa wafa kwa kusombwa na maji ndani ya Noah

Muktasari:

Dereva anadaiwa kukadiria kwa macho maji yenye kasi kwenye daraja la chini, yeye na abiria washindwa kujiokoa

Ruvuma. Watu tisa wamefariki dunia, baada ya gari walilokua wakisafiria kutoka Kijiji cha Tingi kwenda Nyoni kusombwa na maji katika eneo la Lumeme, Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Tukio hilo limetokea jana Machi 11 majira ya saa 12:30 jioni baada ya gari hilo kusombwa na abiria na dereva kushindwa kujiokoa kutokana na maji kuwazidi nguvu na milango kushindwa kufunguka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chillya amethibitisha tukio hilo leo Machi 12, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Songea.

Amesema watu hao walikuwa wakisafiri kwa gari aina ya Toyota Noah, mali ya John Kapinga mkazi wa Kijiji cha Lumecha.

Imedaiwa kuwa dereva gari hilo alilazimisha kuvuka daraja la chini likiwa limejaa maji yaendayo kasi.

Kamanda Chillya, amewataja waliofariki dunia kuwa ni dereva Edwin Ngowoko (55), Valeriana Ndunguru (18), Innocent Kasian (63), Simon Mahai (21)  na Nathan Kumbulu (39).

Wengine ni Faraja Tegete (18), Ebiati Tegete (2), Alfonsia Kasian Mbele (40), Solana Ndunguru (16).

Wakati huo huo, Kamanda Chillya ametoa onyo kwa madereva wa vyombo vya moto kuacha tabia ya kuyakadiria maji kwa macho kwa kuwa ni hatari kwa usalama wa watu, vyombo na mali zao.