TOFAUTI KATI YA MAUZO YA MOJA KWA MOJA NA MFUMO WA MASOKO YA PIRAMIDI UKWELI UKO HAPA

Friday February 05 2021

UKWELI UKO HAPA

Uuzaji wa moja kwa moja una historia ndefu, ikienda mbali katika siku za wafanyabiashara waliosafiri katika miaka ya 1800. Uuzaji huo katika mfumo wa sasa, kama tunavyojua leo umefanywa kuwa maarufu na watuamiaji wa bidhaa za Avon na Amway miaka 60 iliyopita. Lakini tasnia hii inaendelea kujitokeza kutoka kwenye mifumo mingine ya masoko inayoibukia hasa Asia, Mashariki ya Mbali na Afrika. Kwa mujibu habari za uuzaji wa moja kwa moja, Afrika inatajwa kuwa mstari wa mbele katika mfumo wa mauzo ya moja kwa moja, wakati Asia ya Pacific leo inatajwa kuchukua asilimia 44 ya mapato ya mfumo huo ulimwenguni.

Licha ya mfumo wa mauzo ya moja kwa moja kuendelea kukua ulimwenguni, dalili kwamba mfumo huu wa biashara unaoknekana kuendelea kuvutia kwa wajasiriamali, hasa kwenye nchi zenye idadi kubw aya watu ambao hawajaajiriwa na zenye ufinyu wa fursa rasmi za kupata kipato, mfumo huo unapambana na maneno yenye upotoshaji. Hii inatokana na ukweli katika sehemu ya dunia yetu, ambapo uuzaji wa moja kwa moja unachanganywa na mfumo wa piramidi au mifumo ya uwekezaji yenye uhalifu ndani yake.

Katika makala hii, tunajaribu kuelewesha jinsi biashara hii ilivyo na kwa nini inapata upinzani mkali kutoka kwa watu duniani. Kwa kuanzia, ni lazima tuangalie nini maana ya Mauzo ya Moja kwa moja na jinsi yanavyotofautinana na mfumo wa masoko ya Piramidi? Kwa nini kampuni za mauzo ya moja kwa moja kama Amway, Avon, Herbalife, Oriflame, QNET na nyinginezo zinafanyakazi kwa mafanikio katika Bara la Afrika jinsi zinavyotofautiana na mifumo ya Piramidi na Ponzi.

Kwa mujibu wa Shirikisho la la Vyama vya Mauzo ya Pamoja Duniani (WFDSA) “uuzaji wa moja kwa moja ni mkakati wa masoko unaotumiwa na kampuni kubwa ulimwenguni na ndogo za wajasiriamali kutangaza bidhaa na huduma za kutumia moja kwa moja mbali kutoka kwenye kituo cha mauzo ya rejareja. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2019 ya WFDSA), mapato yanayozalishwa na mfumo huo kinasimmia dola za Marekani 180.5 bilioni na kwa makadirio ya wajasiriamali 119.9 milioni wanapata kipato kupitia mauzo ya moja kwa moja, wakiwakilisha baadhi ya bidhaa zinazohitajiwa zaidi za lishe, urembo, bidhaa za nyumbani, vidani, nguo, mapambo ya nyumbani na bidhaa nyinginezo. Ripoti pia inaonyesha kwamba kundi la bidaha zinazouzwa zaidi ni za afya kwa asilimia 36 likifuatiwa na vipodozi na vitu vya kujisafisha na kujiremba kwa asilimia 29.

Mifumo ya piramidi kwa upande mwingine ni kinyume cha sheria na kimzingi huhusisha idadi kubwa ya watu katika sehemu ya chini ya piramidi wakiwalipa hela watu wachache wa juu. Kila mshiriki mpya hulipa kwa lengo la kuendelea juu na kupata faida kutokana na malipo yaw engine watakaojiunga baadaye.

Advertisement

Kulingana na miongozo iliyochapishwa na vyama vya Mauzo ya Pamoja na wataalamu wengine, hapa kuna njia 8 kuonyesha uhalali wa kampuni za mauzo ya moja kwa moja mbali na mifumo ya piramidi.

01. MAUZO YA MOJA KWA MOJA SIYO “MFUMO WA KUTAJIRIKA HARAKA.”

Mauzo ya moja kwa moja yanaweza kuwa ya kuvutia, lakini pia ni biashara ngumu. Kwa kuanzia tu, biashara ya kweli itakwambia kuwa utapata matokeo mazuri utawekeza muda na juhudi zako. Kampuni yoyote inayokuahidi njia nyepesi ya mafanikio unatakiwa kuichukulia tahadhari.

02. KAMPUNI ZA MAUZO YA PAMOJA HULETA BIDHAA NA HUDUMA ZENYE UBORA

Mifumo ya piramidi haina bidhaa wala huduma za uhalali. Kampuni nzuri za mauzo ya moja kwa moja zinahakikisha kuwepo kwa rasilimali za uhakika kufanya utafiti na maendeleo ili kutengeneza bidhaa zenye ubora zilizo halisi za kutumiwa na watu.

03. KAMPUNI ZA MAUZO YA MOJA KWA MOJA ZINA MASHARTI KATIKA MPANGO WAO WA FIDIA

Kapuni za mauzo ya moja kwa moja zinazoheshimika hudhibiti idadi ya watu wanaojipatia kipato cha juu kupitia mauzo. Hiyo ni kwa ajili ya kuweka sawa uwanja wa ushindani kwa wanachama wake. Katika mfumo wa piramidi, ‘mstari wa juu’ au wale watu wa juu waliowahi kushiriki huchukua faida yote, wakati wa ‘mstari wa chini’ au wale wa chini huburuzwa kutokana na kuchelewa kushiriki.

04. WASAMBAZAJI WA MAUZO YA MOJA KWA MOJA HAWAPATI FAIDA KWA KUINGIZA WATU WAPYA

Kuingiza wanachama wapya siyo kigezo cha msambazaji wa mauzo ya moja kwa moja kupata faida. Kampuni halali za maozu ya moja kwa moja zimeundwa kuwafaidia watu wanaotangaza bidhaakatika mfumo wa piramidi hakuna faida ya kifedha mpaka wengine watakapoingizwa.

05. FURSA ZA MAUZO YA MOJA KWA MOJA ZINAMFUMO WA MAFUNZO YANAYOUZWA

Kampuni halali hutoa msisitizo katika mafunzo kwa wasambazaji wao. Wanao wakufunzi waliobobea katika utaalamu na uzoefu kuwasaidia wanachama kuwa na uelewa mzuri wa biashara na bidhaa. Pia wana himiza utamaduni wa kuleana kwa ajili ya kusaidia kukua kwa mtu mmoja mmoja. Kampuni nyingi zilizoanzishwa kama QNET zinamfumo uliofanikiwa wa mafunzo kwa mtu mmoja mmoja na kwa matendo muhimu kwa mamia na maelefu ya wasambazaji duniani kote.

06. FURSA ZA MAUZO YA MOJA KWA MOJA HUJA NA VIFAA VYA KUFANYIA BIASHARA

Kampuni za mauzo ya moja kwa moja zinakuwezesha kutunza na kufuatilia mauzo, faida uliyozalisha na hali ya bidhaa zinazosambazwa pamoja na msaada kwa mteja. Aina nyingine ya msaada ni taarifa za mara kwa mara za bidhaa, zawadi kwa wanaotangaza na vifaa vya masoko ili kuwasaidia wasambaji kuwa na uelewa mzuri wa bidhaa na jinsi ya kuziuza.

07. KAMPUNI ZA MAUZO YA MOJA KWA MOJA ZINA SERA MAHSUSI NA UTARATIBU NA MAADILI YA MASOKO

Kwa uangalifu pitia sera na utaratibu wa kampuni kabla ya kufanya uamuzi. kampuni halali zinalenga kufikia ukuaji endelevu kwa kukuza utamaduni wa maadili ya masoko. Kampuni nyingi za mauzo ya moja kwa moja zina misimamo mkali na inayosimamiwa ili kufikia malengo ya sera, utaratibu na miiko na endapo yakitokea matendo yaliyo kinyume na maadili hatua kali za kinidhamu huchukuliwa haraka.

08. KAMPUNI ZA MAUZO YA MOJA KWA MOJA HAZIENDEKEZI MALIMBIKIZO YA BIDHAA

Kampuni halali za mauzo ya moja kwa moja zinaruhusu wasambazaji kutumia kanuni za kufuata katika shajara na haziruhusu ulimbikizwaji wa bidhaa. Hii inaruhusu wasambazaji kujikita katika mauzo ya moja kwa moja na hivyo kutokuwa na wasiwasi wa ongezeko la bidhaa zilizohifadhiwa.

SABABU ZA MFUMO WA BIASHARA KUANDAMWA

Kuna sababu nyingi zilizochangia kuwepo kwa mchanganyo kati ya mauzo ya moja kwa moja; ya kwanza ni kutokuwepo kwa uaminifu katika biashara, ambapo “Tufaa moja bovu huharibu mzigo wote” ndiyo inavyotawala.

Kampuni zisizo na uaminifu na mtu mmoja mmoja wamekuwa wakijivalisha joho la mfumo wa piramidi na kuufanya kuwa halali.

Sababu ya pili inahusiana na kiwango cha uelewa alionao msambazaji kuhusu kampuni husika au biashara kwa ujumla. Kama msambazaji hana taarifa za kutosha, taarifa anayoitoa kwa wanaotarajia inatia shaka.

Hatimaye, kukosekana kwa kanuni zinazosimamia mfumo kunachangia kwa kiasi kikubwa upotoshaji wa watu kuhusu mauzo ya moja kwa moja. Hata kama mfumo huo kidunia una thamani ya dola za Marekani 180 bilioni, nchi nyingi zinazoendelea hazina sheria ya kuendesha mfumo huo wa biashara.

Hali hiyo inasababisha kapuni zinazofanya mauzo ya moja kwa moja kuchanganywa au kuunganishwa na mifumo ya uwekezaji wa fedha.

Katika nchi nyingi za dunia ya tatu, mtu anaweza kufungwa jela kwa kushiriki mauzo ya moja kwa moja. Kwa mtu anayetaka kujiunga na dunia ya mauzo ya moja kwa moja, kumbuka usichukuliwe na ahadi za uhuru wa kifedha na kufikiwa kwa ndoto zako za muda mrefu.

Mauzo ya moja kwa moja yatakupa mfumo wa biashara, jukwaa na fursa la kujenga mafanikio; hata hivyo, ni jukumu la mtu husika kufanya kazi kwa bidii.


Advertisement