Tozo muamala kutuma au kutoa pesa kutozwa kuanzia Sh10 hadi Sh10,000

Tozo muamala kutuma au kutoa pesa kutozwa kuanzia Sh10 hadi Sh10,000

Muktasari:

  • Serikali imesema itafanya marekebisho kwenye sheria ya Posta na mawasiliano ya kielektroniki kwa kutoza tozo ya Sh10 hadi Sh10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa.

Dar es Salaam. Serikali imesema itafanya marekebisho kwenye sheria ya Posta na mawasiliano ya kielektroniki kwa kutoza tozo ya Sh10 hadi Sh10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa.

Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 10, 2021 na Waziri wa Fedha na Mpango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema pendekezo hilo litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha Sh1.2 trilioni.

“Pia marekebisho yatafanyika na kutoza kiasi cha Sh10 hadi Sh200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha Sh396 milioni,” amesema.