Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TPSF yapongeza bajeti ya Serikali

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024, jijini Dodoma Juni 15, 2023. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Sekta Binafsi imesema bajeti ya Serikali ya mwaka 2023/2024 imezaingatia mahitaji ya Watanzania kwenye sekta zote, japo yapo maeneo yanayotakiwa kufanyiwa kazi.

Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Raphael Maganga amesema bajeti kuu ya Serikali 2023/2024 iliyowasilishwa bungeni Dodoma Juni 15, imezingatia maoni ya sekta binafsi, japo yapo maeneo mengine wana yoendelea kujadiliana na Serikali.

Maganga ameeleza hayo leo Jumatano Juni 21, 2023 wakati akichangia kwenye mjadala wa Mwananchi Twitter Space ulioandliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications L.T.D wenye mada, “Bajeti Kuu ya Serikali 2023/2024 imejibu matarajio ya Wananchi.”

Amebainisha kuwa Sekta binafsi inaongoza kwa kuwa mwajiri mkubwa na ndio mlipa kodi kwa wingi, hivyo ni vizuri Serikali ikaendelea kuwa sikivu kuangalia namna ya kuikuza.

“Bajeti hii imejibu maswali mengi, jambo tulilokuwa tunapigania kwa muda mrefu ni kuona ni kwa namna gani sekta binafsi itakuza uchumi wa Watanzania,” amesema.

Amesema kupitia bajeti hiyo Serikali imeweka mazingira mazuri yatakayodhibiti mfumuko wa bei usipande zaidi ya asilimia 10.  

“Kwa mwananchi wa kawaida kuna ahueni kwenye gharama, tumeona suala la kupandisha bei ya mafuta lakini kwa Tanzania bado bei iko chini ukuilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Wanwake Tanzania, Mwajuma Hamza amesema bajeti imezaingatia mahitaji ya Watanzania kwenye sekta zote japo yapo maeneo yanayoendelea kufanyiwa kazi.

Amegusia miongoni mwa changamoto hizo kuwa ni kuwepo kwa mamlaka za udhibiti nyingi katika sekta ya viwanda, huku pia wafanyakazi wakikatwa kodi nyingi, hali inayochangia kuwepo kwa mianya ya rushwa.

“Tuipongeze Serikali kwa kuja na mfumo wa pamoja wa kutoza kodi, hii itatatua changamoto kubwa ambayo wafanyabiashara walikuwa wanaipata,” amesema.