Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA yashinda tuzo za NBAA kwa mashirika ya umma

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Mcha Hassan Mcha akipokea tuzo ya Ushindi wa kwanza wa jumla katika kipengele cha Uandaaji wa Hesabu za Kifedha zinazozingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha kama mgeni rasmi. katika viwanja vya NBAA Bunju tarehe 4 Desemba, 2025 jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo hutolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Mamlaka ya Mapato tanzania (TRA), imeibuka Mshindi wa kwanza wa jumla katika tuzo ya  Uandaaji wa Hesabu za Kifedha zinazozingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS), zinazotolewa na  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Pia imeibuka mshindi wa kwanza katika tuzo ya kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories) katika tuzo hizo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha Laurent Luswetula,  alizipongeza taasisi zilizoibuka na ushindi, huku akisema wizara hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa NBAA, ili kuendelea kuzalisha wahasibu na wakaguzi bora.

Pia alisema serikali itahakikisha NBAA inasimama imara ili iendelee kuzalisha watendaji bora kwa maslahi mapana ya taifa.

Naye Naibu Kamishina Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha alisema, tuzo walizozipata zina umuhimu mkubwa, kwani zinachangia kuonesha utendaji wa TRA namna unavyokubalika Kimataifa.

Pia alisema tuzo hizo zinaonesha umahiri na ubunifu uliyopo kwa watumishi wa mamlaka hiyo.

"Tuzo hizi zina umuhimu sana kwetu, zinachangia kuonesha utendaji wetu unakubalika Kimataifa na ina waonesha Walipa Kodi kwamba kila shilingi inayokusanywa inafika katika mfuko Mkuu wa Serikali."alisema

Vilevile Naibu Kamishna Mkuu Mcha, aliwashukuru walipakodi kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwasababu TRA imeendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji mapato kwa mwaka wa fedha uliyopita (2024/2025) na kwa mwaka huu wa fedha mpaka kufikia mwezi Novemba, TRA imeendelea kuvuka malengo kwa miezi yote.

"Tunawashukuru sana (walipakodi) kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa Mwaka wa fedha uliyopita ambapo tumevuka malengo, na pia kwa mwkaa huu wa fedha ambao tunakwenda nao tumevuka malengo ya miezi yote mpaka kufikia mwezi Novemba"

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA  Profesa Slyivia Temu,  katika hafla hiyo jumla ya taasisi 86 za Umma na binafsi zimeshiriki katika kujipima ubora wa kuwasilisha taarifa za fedha kwa mwaka 2024.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Pius Maneno, lengo la tuzo hizo ni kuhakikisha taarifa za hesabu zinazotolewa zinakuwa na uwazi na uwajibikaji.

Alifafanua kuwa, tuzo hizo ni taarifa za hesabu za kuanzia Januari mwaka 2024 hadi Desemba, ambazo zimezalishwa kwa kufuata hesabu za Kimataifa na zilizopata hati safi.