Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Transfoma nane za Tanesco zakamatwa Pugu

Transfoma za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), zilizokamatwa maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam zikiwa ndani ya fuso lililoegeshwa katika kituo cha polisi Chanika.

Muktasari:

  • Polisi wapata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, Tanesco yasema kumekuwapo na matukio ya hujumua.

Dar es Salaam.  Transfoma nane  zeye ukubwa tofauti zimekamatwa katika ghala linalohifadhi vyuma chakavu maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam.

Ukamataji wa tranfoma hizo zenye thamani ya Sh94 milioni, umefanyika jana Jumatano Desemba 6, 2023 kwa ushirikiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Jeshi la Polisi na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Ofisa Usalama wa Tanesco Kanda ya Pwani, Lilian William amesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ya kuwepo vifaa hivyo maeneo ya Pugu Dampo katika ghala la vyuma chakavu.

“Tulipofika eneo la tukio tulikuta mmiliki (jina limehifadhiwa) ana vifaa vingi vinavyotumika na Tanesco, tulikuta pia magari yakishusha vifaa vya shirika hili na dereva alipohojiwa alijibu vimenunuliwa Tanga katika mnada.

“Tulipomwambia atupe vielelezo vya ununuzi, tulibaini vilikuwa tofauti na mzigo alioubeba, tulifanya mawasiliano na Tanesco Mkoa wa Tanga ambao walituambia hakuna transfoma walizouza kwenye mnada,” amesema Lilian ambaye pia ni Ofisa Usalama Tanesco Mkoa wa Kinondoni- Kusini.

Amesema wanahisi mali hizo zimeibwa katika maghala za Tanesco kwa sababu taarifa zilizopo ndani ya shirika hilo zinaeleza kuibwa kwa transfoma.

Amesema hivi karibuni kumekuwa na matukio ya hujuma katika shirika hilo katika maeneo mbalimbali ya Pwani na Dar es Salaam, ndio maana Tanesco iliandaa operesheni ya ukaguzi ya kuwabaini watu wanaohujuma na wafanyabiashara wanaojihusisha na ununuzi wa uuzaji wa miundombinu.

Meneja wa NEMC, Kanda ya Ilala Benjamin Dotto amesema walipata wito kutoka Tanesco wa ushirikiano katika mchakato huo, ili kubaini kama taratibu za biashara chakavu zinafuatwa ikiwamo kuwa na vibali vya kukusanya, kusafirisha na kuhifadhi.

“Huyu mmiliki tumemkuta ana vibali vyote, isipokuwa baadhi ya taratibu hazijakaa sawa kwa sababu tulikuta fuso lililobeba transfoma nane katika ghala lake hazina maelezo ya kueleweka.

“Hili pekee tuliona ni jambo la kihalifu hasa Tanesco inavyopata shida ya kuibiwa katika miundombi yake. Tunatoa wito wote wanaojishughulisha na biashara hizi kufuata utaratibu unaotakiwa,”amesema Dotto.

Meneja wa Tanesco wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani, Mhandisi Abdul Mihambo amesema transfoma hizo ni za njia ndogo zinatumika mitaani kupoza na kusambaza umeme kwa wateja.