Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tume ya mipango kuanza kazi Julai mosi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete.

Dodoma. Serikali imesikia kilio cha wabunge waliotaka irejeshwe tume ya Taifa ya Mipango ikibainisha kwamba itaanza kazi yake Julai Mosi, 2023.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 20, 2023 wakati akijibu swali la mbunge wa Mlalo (CCM) Rashid Shangazi.

Shangazi amehoji ni lini Serikali itafufua upya tume ya Taifa ya Mipango ambapo akijibu swali hilo, Ridhiwan amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya muswada wa sheria ya kuanzisha tume hiyo.

“Muswada huu unatarajiwa kuwasilishwa bungeni katika mkutano wa 11 unaoendelea sasa na ukipitishwa, tume hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake katika mwaka wa fedha 2023/2024 yaani Julai Mosi 2023.