Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tume yabaini viongozi wa kisiasa kutumia dola kukamata watu

Dar es Salaam. Tume ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini imebaini baadhi ya viongozi wa juu wa siasa kuingilia mnyororo wa haki jinai kwa kuamuru vyombo vya dola kukamata na kuwaweka ndani mwananchi wakati mamlaka hayo hawana.

Akisoma taarifa rasmi ya tume hiyo leo Jumamosi Julai 15, 2023 Ikulu, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Jaji Mstaafu, Othman Chande amesema viongozi hao waelekezwe kuzingatia sheria.

“Tume imebaini kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa siasa wamekuwa wakitoa matamko na amri za kuamuru vyombo vya dola kukamata na kumweka ndani mwananchi wakati mamlaka hayo hawana, hivyo viongozi hao waelekezwe kuzingatia sheria”

Tume ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Januari 2023 na kuanza kazi Februari Mosi.