Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Turkish Airlines yarejesha safari zake Tanzania

Muktasari:

  •  Shirika la Ndege la Turkish Airlines la nchini Uturuki ambalo lilisitisha safari zake nchini 2020 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19 limetangaza kurejesha na safari zake June 2022 .

  


Hai. Shirika la Ndege la Turkish Airlines la nchini Uturuki ambalo lilisitisha safari zake nchini 2020 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19 limetangaza kurejesha na safari zake June 2022 .

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Christine Mwakatobe wakati aakieleza uongozi wa kiwanja hicho cha ndege (KADCO) ulivyopokea tuzo ya umahiri wa rasilimali watu katika uwakilishi wa wanawake kwenye ngazi ya Menejimenti.

Amesema shirika hilo litakuwa linafanya safari zake mara nne kwa wiki kupitia uwanja wa KIA.

"Menejimenti  ya KADCO kwa kushirikiana na wadau mwaka huu wa fedha ambao tupo sasa tumefanikiwa pakubwa  sana, Mwezi Oktoba mwaka jana tulipokea Shirika la ndege la Ederecy kutoka Zurich kuja Kilimanjaro ambalo  linakuja mara mbili kwa wiki, June 4 mwaka huu tutapokea tena shirika la ndege jipya la  Eurowings discover ambalo litakuwa linatoka Frankfurt  Mombassa kuja Kilimanjaro.

"June 20, 2022 Shirika la Ndege la Uturuki, Turkish Airlines ambalo lilisitisha safari zake mwezi Machi, 2020 wakati wa ugonjwa wa Uviko  19  litaanza kurudi tena rasmi  mara nne kwa wiki,"amesema Mwakatobe

Amesema kurejea kwa mashirika hayo hapa nchini ni mafanikio katika uwanja huo wa ndege wa KIA ambapo amesema ni wakati mwafaka hasa katika uzinduzi wa Royal Tour ambao umefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii duniani.