Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchaguzi KKKT: Askofu Bagonza aibuka na mambo matatu

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza.

Muktasari:

  • Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza amezungumzia siku nne za mkutano mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ulioanza Agosti 21 hadi 24, 2023 uliofanyikia Chuo Kikuu cha Tumain-Makumira (Tuma) jijini Arusha.

Dar es Salaam. Baada ya mkutano mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kumalizika kwa kupata Mkuu wa kanisa hilo mpya, Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza ameibuka na mambo matatu.

 Askofu Bagonza ameeleza mambo hayo baada ya juzi usiku Alhamisi Agosti 24,2023 kuhitimishwa kwa uchaguzi ambapo Askofu Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani kuibuka mshindi wa Mkuu wa KKKT akichukua nafasi iliyoachwa na Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozi.

Shughuli za uchaguzi na mambo mengine ikiwemo mabadiliko ya katiba ya KKKT zilianza Agosti 21, 2023 kwa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini Tanzania.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni mbalimbali nje ya KKKT akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi na kufanyikia Chuo Kikuu cha Tumain- Makumila (Tuma) jijini Arusha.

Katika uchaguzi huo uliokuwa na ulinzi na waandishi kutokuruhusiwa kuingia, maaskofu wawili, Dk Bagonza na Ambele Mwaipopo wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika waliondolewa ukumbini kabla ya shughuli ya uteuzi wa majina ya wagombea na upigaji kura kufanyika.

Askofu Mwaipopo na Bagonza walisimamishwa kuhudhuria vikao vinne vya kawaida vya Halmashauri Kuu Mei 2022 kwa kutofautiana na mkuu wa Kanisa, Askofu Fredrick Shoo juu ya namna ya kushughulikia mgogoro wa Dayosisi ya Konde uliokuwa ukiendelea.

Mwananchi Digital lina taarifa kuwa, katika kikao cha Halmashauri Kuu kilichokutana kabla ya kikao cha uteuzi, Askofu Bagonza na Mwaipopo walisamehewa kwa sharti la kutakiwa kuandika barua ya kuomba radhi ambapo walitekeleza.

Hata hivyo, Askofu Shoo aliibua hoja akisema maaskofu hao walitakiwa kuandika barua na wakaandika ila alikuwa bado hajaziona hivyo hawawezi kuwepo kwenye kikao hicho. Wawili hao walitakiwa kutoka ukumbini ili wajadiliwe.

Baada ya kujadiliwa, maaskofu hao hawakuruhusiwa kurudi ukumbini na shughuli ya uchaguzi ikaendelea na Mwananchi Digital lina taarifa kati ya majina matano yaliyoteuliwa kugombea Askofu Bagonza alikuwa miongoni mwao akipata kura 15 sawa na alizopata Askofu Andrew Gulle.

Aliyewaongoza alikuwa Askofu Abednego Keshomshahara  kura 32, Askofu George Fihavango kura 20 na  Askofu Malasusa aliyepata kura 16.

Baada ya yote hayo, Askofu Bagonza ametumia kurasa zake za kijamii, kuandika ujumbe wenye mambo matatu ya kufikirisha akiupa kichwa cha habari 'hatugombei, tunagombezwa.'


Ujumbe huo wa Askofu Bagonza unasema:

Wapendwa wangu, nimejizuia sana kuandika au kusema chochote. Lakini mmenisonga sana, nami nimo safarini. Kwa kuwa sijui kama nitafika niendako (Vienna) kabla hamjakata tamaa na kuzimia, naomba msome kwa furaha mambo haya matatu:

1. Tumetazamwa na dunia nzima kwa siku nne. Mmoja aliyeona na alikuwa mgeni akaniuliza: “Hivi nyie wenzetu Wachungaji na Maaskofu mmeishagundua mbingu haipo mkafanya iwe siri yenu tu?” Akaongeza, “kama mbingu ipo kwa nini mfanyiane haya mabaya hadharani?

2. Nilizoezwa kuamini kuwa watu wanakataliwa kwa sababu ya ubaya wao na wengine hupendwa kwa sababu ya uzuri wao. Sasa nimeamini wapo wanaoweza kukataliwa kwa uzuri na wakapendwa kwa ubaya wao. Cha msingi, ubaya hauwezi kukaa kwa amani na wema. Tumefundishwa:

Katika Agano la Kale, kichafu kikigusana na kitakatifu, kile kitakatifu kinaharibika.

Katika Agano Jipya, kichafu kikigusana na kitakatifu, kile kichafu kinatakasika. TKKK ni ya Agano Jipya au la Kale?

3. Watu wakatili na waovu hujiandaa kupiga na kuangamiza wabaya wao wakati wote. Watu wema hutafuta kuushinda ubaya kwa wema.

Hutokea wakati, wapigaji wakapiga na kufurahi kuwa wamepiga. Wakitulia hugundua kuwa kumbe wamepigwa sana. Kutosamehe ni sawa na kunywa sumu ukitegemea afe adui yako. Sumu uliyokumywa bila kukusudia inaua vibaya.

Humu kibandani kwetu huwa hatugombei bali tunagombezwa na kuzodolewa.

Unione nitakapokuona.