Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukatili wa kingono waponza wawili, kutumikia kifungo jela

Muktasari:

  • Hukumu hiyo imesomwa Julai 20,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela, baada upande wa Jamhuri kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Kyela. Mahakama ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imewahukumu wanaume wawili kutumikia jumla ya miaka 50 jela baada ya kupatikana na hatia ya kutenda makosa ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto katika matukio tofauti.

Katika shauri la kwanza, Mahakama imemhukumu Paulo Mwakaluwa (46), mkazi wa Kijiji cha Ikombe kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10, mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikombe.

Hukumu hiyo ilitolewa Julai 20, 2026 na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kyela, Paulo Barnabas baada ya kuridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha shtaka hilo kupitia ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo

Kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa mashtaka, mshtakiwa alitenda kosa hilo katika nyakati tofauti, Agosti 2025, baada ya kumkuta mtoto huyo akitoka shuleni na wakati mwingine akiwa njiani kuelekea ziwani.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa katika moja ya matukio hayo, Barnabasi alimpeleka mtoto huyo nyumbani kwake ambako alimbaka, kisha akamtishia kumuua endapo angeeleza yaliyotokea.

Akiwasilisha hoja za mwisho, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wakili Sharon Sekemi, aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Mahakama ilimhukumu Mwakaluwa kifungo cha miaka 30 jela na kumweleza kuwa ana haki ya kukata rufaa ikiwa hajaridhika na hukumu hiyo.

Katika shauri jingine, Mahakama hiyo imemhukumu Amani Mwalupeto (30), mkazi wa Ipinda wilayani Kyela, kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya shambulio la aibu dhidi ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne, Julai 21, 2026 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kyela, Rosta Mofuga baada ya kuridhika kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ulithibitisha shtaka hilo bila kuacha shaka.

Mahakamani ilielezwa kuwa Desemba 18, 2025, Mwalupeto alimkuta mtoto huyo akicheza na wenzake, kisha akampandisha kwenye baiskeli kwa madai kuwa walikuwa wanakwenda kuokota maembe.

Ilidaiwa kuwa alipofika naye eneo la vichaka, alimfanyia shambulio la aibu kwa kumwingizia vidole sehemu za siri na baadaye akamtishia kwa kumuonya asimweleze mtu yeyote kuhusu tukio hilo.

Katika shauri hilo pia, Wakili Sekemi aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wahalifu wengine na kuchangia juhudi za kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa, Mahakama imemhukumu Mwalupeto kutumikia kifungo cha miaka 20 jela.