Ukweli kupanda bei ya mafuta kujulikana Septemba 16

Ukweli kupanda bei ya mafuta kujulikana Septemba 16

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema kamati iliyoundwa kuchunguza kupanda kwa bei ya mafuta itawasilisha ripoti yake kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 16, 2021.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema kamati iliyoundwa kuchunguza kupanda kwa bei ya mafuta itawasilisha ripoti yake kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 16, 2021.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumamosi Septemba 4, 2021 msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kamati hiyo iliyoundwa Septemba 2,   2021 imepewa wiki mbili kukamilisha kazi hiyo.

Amesema itaangalia tozo zilizopo kwenye mafuta, kampuni zinazoagiza mafuta kuja nchini na utaratibu uliowekwa katika Bandari ya Dar es Salaam na Mtwara ili kujua sababu za kupanda kwa bei hiyo.


“Serikali inaangalia kupanda kwa mafuta kama kuna maeneo yanayoweza  kushughulikiwa ili Watanzania waendelee kupata mafuta kwa bei ya chini,” amesema.

Amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwa kuwa kupanda bei kwa nishati hiyo kuna.madhara katika maisha ya kila siku na kwenye uchumi.