Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulanga: Tanzania inahitaji viongozi kusimamia uchumi

Mjumbe Bodi ya Taasisi ya Strathmore Global Institute (SGI), John Ulanga akichangia mada katika uzinduzi wa taasisi hiyo inayotoa mafunzo ya uongozi, jijini Dar es Salaam jana.

Dar es Salaam. Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali wenye uzoefu wameshauriwa kusoma masomo ya uongozi, kutokana na mabadiliko yaliyopo, yakiwemo ya kiuchumi na kiteknolojia.

Kutokana na mabadiliko hayo, Tanzania itahitaji viongozi watakaoweza kuongoza, kampuni na taasisi za ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jana Julai 19, 2023 wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Strathmore Global Institute inayotoa mafunzo ya uongozi nchini, Mjumbe wa bodi ya taasisi hiyo, John Ulanga alisema endapo watu hawatasoma baadaye athari yake inaweza kuonekana.

"Tanzania inahitaji kuwa na viongozi wengi wenye uwezo wa kuongoza kampuni na taasisi za ndani na nje kutokana na ukuaji wa uchumi kwenye sekta mbalimbali," amesema.

"Pia tunahitaji kuwa na timu ya viongozi zaidi ya 1,000, watakaoweza kuongoza kampuni na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi,"

Alibainisha kutokana na ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha miaka mitano hadi 10 ijayo, uchumi utakua umeongezeka kwa kasi hasa kwenye sekta zikiwemo usafirishaji, madini mafuta na gesi pamoja viwanda na ujenzi.

Akizungumzia taasisi hiyo Ulanga alisema, itatoa mafunzo kwa watu wenye uzoefu wa kazi na kutaka watu mbalimbali kupata mafunzo hayo.

Kuhusu mabadiliko ya tabianchi alisema, endapo watu wataitumia taasisi hiyo kujiendeleza, Tanzania itakuwa na wataalamu wengi watakaoweza kuisaidia.

 "Kutokana na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, tunahitaji viongozi watakaoweza kusimamia mifumo na uzalishaji wa chakula, kuhakikisha Serikali na sekta binafsi wanakuwa na mikakati bora," amesema.

Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Kiongozi, Emma Kawawa alisema kutokana na changamoto ya ajira, watu wanahitaji kuwa na ujuzi ili waweze kusimamia biashara na shughuli zao, huku akibainisha kuwa kwa sasa taasisi hiyo imejikita katika kutoa elimu na mafunzo ya uongozi.

Awali, Meneja wa taasisi hiyo nchini, Tatiana Mengsen alisema taasisi hiyo yenye miaka zaidi ya 60, ina makao yake nchini Kenya.

Alibainisha kuwa madhumuni ya kuanzishwa kwa taasisi, ni ili kutoa mafunzo ya namna kuwa kiongozi.

"Tumeamua kufungua tawi lingine ili kuwafikia Watanzania kwa ukaribu, lakini sio tu kwa ajili ya viongozi. Mafunzo hayo yatasaidia pia watu wanaotaka kuanza biashara,' amesema.