Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulevi unavyoitesa Rombo

Muktasari:

  • Kanisa limeingilia kati na kushindwa, waiomba Serikali kukomesha hali hiyo

Rombo. Kuendelea kukithiri kwa unywaji na uuzwaji wa pombe ya moshi maarufu kama gongo, kumeendelea kuitesa wilaya ya Rombo baada ya baadhi ya wanafunzi kujihusisha na unywaji wa pombe hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa dini na wananchi, walisema kuendelea kwa unywaji wa pombe hiyo kumeathiri nguvu kazi ya Taifa.

Paroko wa Usseri, Padri Emmanuel Lyimo alisema Taifa linapoteza vijana wanaotegemewa kukuza uchumi kutokana na watu ambao hawana nia njema ambao wamekuwa wakifanya biashara ya gongo.

Padri Emmanuel alisema kutokana na Serikali kuwa na mkono mrefu isaidie kupunguza hali hiyo ambayo inaendelea kuumiza vijana wengi wadogo.

“Sasa hivi wanafunzi nao wamejiingiza katika unywaji na uuzaji wa gongo, wengi hawaendi shule kutokana na kuathirika na ulevi na vijana wameshindwa kuoa kutokana na ulevi,” alisema.

Mwaka juzi, wanawake wa wilaya hiyo walilalamika waume zao kupoteza nguvu ya kujamiiana kutokana na unywaji gongo.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Sango, Genes Kimario, alisema matukio hayo yameendelea kuitesa jamii kutokana na vijana wengi wakitoka shule hawana kazi za kufanya na kujikita katika unywaji wa pombe.

Kimario alisema hali hiyo imeshindikana kudhibitiwa kwa kuwa watu wenye fedha wanaojuana na viongozi wakubwa huingilia kati.

Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Rombo, Agness Hokororo, alisema hana taarifa kama wanafunzi nao wamejiingiza katika unywaji wa gongo.