Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UN, AKDN wadau kuisaida Tanzania kuwezesha vijana

Muktasari:

  • Ili kuwaandaa vijana ili waweze kuchangamkia kikamilifu fursa zilizopo, Umoja wa Mataifa (UN) na wadau wamejitolea kuisaidia Tanzania kukamilisha azma hiyo.

Dar es Salaam. Umoja wa Mataifa, wadau mbalimbali wa maendeleo ukiwemo Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) wamejitolea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuwezesha vijana ili kuweza kupata kizazi kitakachosaidia taifa la kesho.

Hilo linafanyika ili kuendana na kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa inayofanyika kila Oktoba 24 isemayo 'wekeza leo kwa ajili ya kesho kwa kuinua vijana wa Kitanzania'.

Akizungumza katika siku ya Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Taasisi ya  Elimu ya Aga Khan Tanzania (AKEST), Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu (Unesco) Michel Toto amesema hilo litafanyika kwa kutengeneza mazingira rafiki.

"Mazingira hayo ni yale yanayoruhusu uvumbuzi, ujasiriamali na ushiriki wa vijana katika michakato ya kufanya maamuzi ambayo yana tija kwenye maisha yao na hatma yao kwa ujumla," amesema Toto.

Amesema wakati wakisherehekea maadhimisho hayo ni vyema kukumbuka kuwekeza kwa vijana wa Tanzania, siyo tu kwa ajili ya kuchagiza siku zijazo bali  kujenga jamii inayojumuisha zaidi usawa na uendelevu kwa wote.

Amesema kuwekeza katika vijana ni kuwekeza katika maendeleo ya Taifa huku akieleza kuwa hilo linawezekana kwa kuwapa stadi, maarifa, na fursa wanazohitaji kwani ndiyo zinawafanya kuwa washiriki hai katika kujenga ulimwengu bora na endelevu zaidi.

"Hii ikiwa inamaanisha kutoa elimu bora, kukuza fursa za uwezeshaji, na kukuza mazingira ambayo sauti zao zinasikika, na maoni yao yanathaminiwa," amesema Toto.

Amesema Tanzania ni sawa na nchi nyingine duniani ambazo idadi ya vijana sio tu ni faida kwa wakati ujao lakini ni nguvu inayoongoza kuwa nyuma ya maendeleo ya taifa.

Dk Shelina Walli ambaye ni Mkurugenzi wa AKEST, amesema wameandaa maadhimisho ya umoja wa mataifa kwa sababu wanataka elimu wanayoitoa kwa wanafunzi iendeleze usawa, uvumilivu na vitu ambavyo wanataka kuona kwa jamii ijayo.

"Sisi tunaona wanafunzi wetu ni viongozi wetu, siyo viongozi wa kesho ila wa leo kwani wanatuongoza kujifunza na kutusaidia sisi tujifunze jinsi maisha yanaweza kuendelea kwa upendo, amani na haki za binafamu wote," amesema Dk Walli.