Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upelelezi vigogo Acacia wasubiriwa kutoka nje

Aliyekuwa Makamu Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia, Deogratius Mwanyika (kulia) na meneja mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo wakiwa katika katika mahakama ya kisutu.

Muktasari:

  • Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia, Deogratius Mwanyika na wenzake bado haujakamilika na wanasuburi msaada wa kisheria kutoka nje ya nchi.

Dar es salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Makamu Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia, Deogratius Mwanyika na wenzake bado haujakamilika na kinachosubiriwa ni msaada wa kisheria kutoka nje ya nchi.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi zaidi ya Dola112 milioni.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Ijumaa Machi 29, 2019 kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa hivyo wanaendelea kufuatilia msaada wa kisheria nje ya nchi na bado hawajapewa majibu.

"Tunaendelea kufuatilia ili kujua maendeleo ya upelelezi, nimeomba siku chache kuhusiana na uchunguzi hivyo siku ya shauri hilo nitawajulisha nimefikia wapi," amedai Wankyo.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina alisema upande wa mashtaka watakapokuja kwa ajili ya kesi hiyo wawajulishe upelelezi umefikia wapi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 4, 2019 itakapokuja tena kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Mbali na Mwanyika washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni meneja mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo, mkurugenzi mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhulu Assa Mwaipopo, kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, saba ya kughushi, 17 ya utakatishaji fedha, kuwasilisha nyaraka za uongo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa, mashtaka nane ya kukwepa kodi na moja la kutoa rushwa.

Wanadaiwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11, 2008 na Juni 30, 2007 katika sehemu tofauti Jijini Dar es Salaam, Kahama mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maeneo mengine ambayo washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo ni katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini Uingereza.

Aidha Mwanyika na Lugendo, wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutoa tamko la uongo kwa kamishna jenerali wa TRA huko Biharamulo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi ya Dola9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa TRA.

Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kuwa kati ya Desemba 2009 na Desemba 31, 2018 katika maeneo tofauti ndani na nje ya Tanzania kwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani, walisaidia mgodi wa North Mara kuhamisha fedha kiasi cha Dola 374,243,943,45 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa ya kughushi na kukwepa kodi.

Pia washtakiwa wanadaiwa kati ya Novemba 2, 2012 na Novemba 27, 2015 huko Shinyanga walitoa rushwa ya Sh718,520,001.76 kwa Hussein Kashindye ambaye ni mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoani Shinyanga ili kumshawishi aachane na uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyokuwa yametendwa na Mgodi wa Bulyanhulu.

Katika shtaka la kughushi washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai waligushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30, 2014 Kampuni ya Pangea Limited ilikubali kukopa Dola90,000,000 ikiwa na riba kutoka Benki ya Barrick huku wakijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la kutoa nyaraka ya uongo, Mwanyika anadaiwa Aprili 30, 2018 huko BOT wilaya ya ilala, kwa makusudi aliwasilisha nyaraka ya uongo za mkopo baina ya kampuni ya mgodi wa Bulyanhulu na Barrick International Bank Corp kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, kati ya Juni 2001 na Desemba 13, 2007 Bulyanhulu walijipatia mkopo usio na faida wa Dola 416,100,000 kutoka Barrick.