Utapiamlo unaathiri uzalishaji, uchumi, ni muda wa kuwekeza katika lishe sasa

Saturday August 06 2022
New Content Item (1)

Mhudumu wa afya akimsaidia mama kumnyonyesha mwanae. Picha na UNICEF Tanzania.

Na Dk Sophie Tadria

Kila mwaka, Serikali hutumia matrilioni ya dola katika gharama za huduma za afya kuto­kana na utapiamlo wa aina zote.

Utapiamlo ni upun­gufu au ziada ya ulaji wa virutubisho, ukosefu wa ulinganifu wa viru­tubisho muhimu au matumizi ya virutubisho venye dosari.

Utapiamlo umekuwa na gharama kubwa za kijamii na kiuchumi kwa watu binafsi, hususan watoto wadogo, wasi­chana waliofikia balehe, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, wazee, wagonjwa na wenye kinga dhaifu, pamoja na familia na jamii.

Pia athari zake nyingine zinaonekana dhahiri katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi, inakwamisha uwezo wa binadamu, maendeleo ya kiakili na kimwili, huhatarisha kinga na huongeza uwezekano wa magonjwa.

Utapiamlo unatara­jiwa kuongezeka kuto­kana na athari za kiuchu­mi za janga la Uviko-19 na vita vinavyoendelea nchini Ukraine, ambavyo vinaharibu mnyororo wa ugavi na kupandisha bei ya nafaka, mbolea na nishati.

Advertisement

Kwa mujibu wa ripoti ya Hali ya Dunia ya Usal­ama wa Chakula na Lishe ya 2022 iliyotolewa hivi karibuni, idadi ya watu duniani kote ambao hawawezi kumudu lishe bora iliongezeka kwa milioni 112 na kukaribia kufikia hadi bilioni 3.1, ikionyesha athari za kupanda kwa bei ya vyakula katika uwezo wa kumudu milo kamili.

Faida ya uwekezaji katika lishe

Uwekezaji katika lishe bora una moja ya faida kubwa zaidi kwenye uwekezaji katika suala la maendeleo na ustawi wa binadamu.

FAO, kwa mfano, iliko­kotoa kuwa uwekezaji wa kila mwaka wa dola za Marekani bilioni 1.2 katika kuboresha ugavi wa virutubisho vidogo vidogo duniani ungesa­babisha “afya bora, vifo vichache, na ongezeko la mapato kwa siku zijazo” ya hadi dola bilioni 15.3 kwa mwaka: uwiano wa faida dhidi ya gharama kuanzia 13 hadi 1.

Kuwekeza katika lishe bora huchochea ukuaji wa uchumi, kuboresha ustawi wa binadamu na usawa, kusaidia uende­levu wa mazingira na kuimarisha uhimilivu wa familia na jamii.

Ingawa gharama za kukabiliana na athari za utapiamlo ni kubwa, iwe katika masuala ya fedha, kiuchumi au kibinad­amu, gharama ya kujik­inga dhidi yake ndogo zaidi.

Ni wazi kwamba ili kukuza mifumo ya lishe yenye ulinganifu zaidi, si tu tutoe chakula zaidi, bali pia vyakula bora na nafuu zaidi kama vile vyakula vinavyotokana na wanyama, jamii ya kunde, na mboga mboga na matunda fulani.

*Ofisa Sera wa Mradi wa FIRST, FAO Tan­zania

Advertisement