Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utata mwanamke anayedaiwa kumuua mwanaye na kumzika

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa

Muktasari:

  • Hakika ukishangaa ya Mussa Utaona ya Firauni, ndiyo ambavyo unaweza kusema kwa tukio linalodaiwa kufanywa na a Rebbeca Siowi (30),mkazi wa kijiji cha Makiwaru mkoani Kilimanjaro.


Siha. Hakika ukishangaa ya Mussa Utaona ya Firauni, ndiyo ambavyo unaweza kusema kwa tukio linalodaiwa kufanywa na a Rebbeca Siowi (30),mkazi wa kijiji cha Makiwaru mkoani Kilimanjaro.

Siowi anatuhumiwa kumuua mwanaye mwenye ulemavu kwa njaa , Salah Jackson (5) na kisha kumzika kimya kimya.

Mwanamke huyo mwenye watoto sita anadaiwa kumzika mwanaye huyo Aprili 21 mwaka huu nyumbani kwa wazazi wake bila yeyote miongoni mwa jamaa na ndugu zake, ndipo baadaye Jeshi la Polisi lilipata taarifa hizo kutoka kwa wananchi ambapo mwili huo ulifukuliwa jana Aprili 22.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo.

“Hili tukio kweli lipo na baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa juu ya tukio hilo tulikwenda kuomba kibali cha kufukua mwili ili kujiridhisha sababu za kifo cha mtoto huyo ni nini kutokana na maneno mengi yaliyokuwepo mtaani,”alisema Kamanda Maigwa

“Tulifukua mwili jana na kuupeleka hospitali kwa uchunguzi na majibu ya daktari yalionyesha mtoto huyo alikufa kwa njaa, kwa hiyo hakuna tunayemshikilia na tukio la mauaji maana imethibitika mtoto alikufa kwa njaa,”alisema Kamanda Maigwa

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Makiwaru, Barakaeli Nasari alisema alipata taarifa kutoka kwa bibi wa mtoto huyo kuwa mjukuu wake haonekani na ndipo baadaye ilibainika kuwa amezikwa na mama yake bila kuambiwa.