Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Aga Khan, Elekta kununua vifaa matibabu ya saratani

Muktasari:

  • Taasisi ya Aga Khan Tanzania na shirika la Elekta wametiliana saini mkataba wa ununuzi na uwekaji wa vifaa tiba ya saratani.

Dar es Salaam. Taasisi ya Aga khan Tanzania na shirika la Elekta wametiliana saini mkataba wa ununuzi na uwekaji wa vifaa tiba ya saratani kwa njia ya mionzi katika kituo cha huduma za saratani jijini hapa.
Taasisi hizo zimenunua vifaa hivyo kupitia Mradi mtambuka wa saratani Tanzania (TCCP) inatarajia kununua kifaa cha kisasa cha tiba ya mionzi na vifaa vingine vinavyohusisha matibabu hayo.
Vifaa hivyo vinavyotoka nchini Sweden vitafungwa katika hospitali ya Aga Khan na kuifanya kuwa hospitali ya kwanza nchini na ya pili Afrika Mashariki na Kati kuwa na teknolojia hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, leo Januari 16, 2023 Meneja wa TCCP, Dk Harrison Chuwa, amesema kifaa kitakachofungwa kitaongeza kasi ya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi.

Aga Khan, Elekta kununua vifaa matibabu ya saratani


"Kifaa hicho kinaruhusu mbinu za aina zote za matibabu kupitia tiba ya mionzi (3D, CRT, VMAT, IMRT) na kujumuisha upasuaji kwa njia ya mionzi kwa uvimbe mdogo ambao uhitaji matibabu ya mionzi ya uhakika,” amesema.
Hata hivyo, amesema wanatarajia baada ya vifaa kuwasili Mgonjwa wa kwanza ataanza kutibiwa mwakani.
"Bei ya kifaa hicho ni takribani Euro 4.5 million sawa na Sh11.4 bilioni na kitahudumia watu 50 kwa wastani au zaidi ya hapo,” amesema.  
Makamu wa rais, kutoka Elekta Feras Al Hasan, yeye amesema " kwenye kampuni ya Elekta wana kusudi moja ambalo linawapa motisha kama kampuni na kama mtu binafsi, matumaini kwa kila mtu anayehusika au kuguswa na saratani,
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Tiba na Afya, Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan Dk Gijs Walvaren amesema lengo lao linabakia katika kukuza ubora wa utoaji wa huduma za afya na usalama wa wagonjwa na kuongezeka kwa upatikanaji kutoka huduma.